Handala hivi karibuni pia walidukua simu ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Naftali Bennett, na kutoa nyaraka na picha za kiongozi huyo, hatua inayoongeza wasiwasi kuhusu usalama wa mawasiliano ya viongozi wa Israel.

29 Desemba 2025 - 00:46

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- linaripoti kuwa kundi la wadukuzi linalojitambulisha kama Handala, lenye uhusiano na Iran, limedukua simu ya Iphone 16 Pro Max ya Tzachi Braverman, mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Kundi hilo limedai kuwa limefanikiwa kuingia kwenye simu hiyo kwa muda mrefu bila kugundulika na kukusanya taarifa nyeti, ikiwemo mawasiliano ya faragha, makubaliano ya siri, matumizi mabaya ya madaraka, na nyaraka zinazohusiana na uongozi wa juu wa Israel.

Handala wamesema Braverman, anayechukuliwa kuwa mmoja wa watu wa karibu sana na Netanyahu, alikuwa akihifadhi siri nyingi za kisiasa na kiusalama. Kundi hilo limeonya kuwa lina mpango wa kuanika nyaraka, sauti, na video zinazohusiana na kile wakiita “Bibi Gate,” kashfa inayodaiwa kuhusisha ufisadi na mahusiano ya siri ya kisiasa.

Serikali ya Israel bado haijatoa tamko rasmi kuthibitisha au kukanusha madai haya, huku madai haya yakiwa yamesababisha mjadala mkubwa kuhusu usalama wa mawasiliano ya viongozi wa ngazi ya juu wa serikali. Kundi la Handala linahusishwa moja kwa moja na idara za usalama na ujasusi wa Iran, huku likiwa lilishiriki katika uvujaji wa kashfa ya “Qatargate” iliyowezesha uchunguzi wa mahusiano ya siri kati ya Netanyahu na serikali ya Qatar, jambo lililochochea maandamano makubwa nchini Israel.

Aidha, handala hivi karibuni pia walidukua simu ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Naftali Bennett, na kutoa nyaraka na picha za kiongozi huyo, hatua inayoongeza wasiwasi kuhusu usalama wa mawasiliano ya viongozi wa Israel.

Your Comment

You are replying to: .
captcha