Haki
-
Bondia Muhammad Ali: "Ikiwa unataka kuuelewa Uislamu, basi kwanza jifunze uelewe tukio la Karbala"
Muhammad Ali - Bondia maarufu wa wakati wote alitoa kauli hiyo mwaka 1993 katika Mwezi kama huu wa Muharram ambapo naye alishiriki katika Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as).
-
Mimbari ya Imam Hussein (as) - Nchini Malawi | "Tofauti kati ya Mtu anayemjua Imam Hussein (AS) na Asiyemjua Imam Hussein (as)"
Sheikh Abdul Rahman Kachere: "Mtu anayemfahamu Imam Hussein (AS) daima ni jasiri katika kukabiliana na dhulma".Kumjua vizuri Imam Hussein (as) kutawafanya watu wa mataifa mbalimbali kumpinga adui na dhalimu, na kutambua njama za adui na dhalimu dhidi ya mataifa yao, na kuwa tayari kupambana kwa ajili ya kuinusuru Haki, kwa ajili ya kuondoa uistikbari, dhulma na unyonyaji wa mfumo mpya wa ukoloni unaoitwa: Ukoloni mambo leo.
-
Falsafa ya Maombolezo na Kumbukumbu ya A'shura | Kulinda Haki na Uhuru wa Watu ni Muhimu zaidi kuliko Maisha binafsi
Haki ya mtu binafsi na umma: Imam Hussein alijua kwamba alikuwa akielekea kifo, lakini alikusudia kuonyesha ulimwengu kuwa kulinda haki na uhuru wa watu ni muhimu kuliko maisha binafsi. Maombolezo ya Ashura yanatufundisha kuwa watu wanapaswa kuwa tayari kujitolea, si tu kwa ajili ya nafsi zao, bali kwa ajili ya ustawi wa jamii.
-
Venezuela: Dunia imefurahishwa na pigo Kali la Iran dhidi ya Utawala wa Kizayuni
Waziri Mkuu wa Venezuela l: "Venezuela inasimama bega kwa bega na Iran katika Haki yake ya kujihami na kuilinda amani yake dhidi ya majaribio yoyote ya jinai za kizayuni".
-
Araghchi: "Kiongozi Mkuu ameweka wazi wajibu wa Iran kuhusu urani na kwamba suala la urutubishaji wa Urani (uranium enrichment) halipo mezani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqhchi, alizungumza kuhusu msimamo wa Marekani katika mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza kwamba suala la urutubishaji wa urani (uranium enrichment) halipo kabisa katika meza ya majadiliano. Alisema kuwa urutubishaji si jambo ambalo linapaswa kujadiliwa, kwani haki ya Iran ya kuendeleza mpango wake wa nyuklia ni jambo la msingi na lililowekwa wazi. Aidha, aliongeza kuwa: Kiongozi Mkuu alisema wazi kuhusu hili katika majadiliano yaliyopita na hakubali kuona suala hili likiingizwa tena katika mchakato wa majadiliano.