24 Desemba 2025 - 18:47
Araqchi: Marekani Haitaki Diplomasia ya Kweli, Bali Kulazimisha Iran Kunyimwa Haki Zake

Araqchi: "Diplomasia ya kweli haiwezi kujengwa juu ya mashinikizo na masharti ya upande mmoja. Kuitaka Iran iachane na haki zake halali si mazungumzo, bali ni jaribio la kulazimisha,”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araqchi, amesema kuwa Marekani imekuwa ikitoa tafsiri mpya ya diplomasia inayolenga kuilazimisha Iran iachane na haki zake halali, akisisitiza kuwa hali hiyo haiwezi kuitwa mazungumzo ya kweli.


Araqchi ameeleza kuwa kile kinachowasilishwa na Marekani kama diplomasia si chochote zaidi ya kulazimisha na kuamrisha, badala ya kujengwa juu ya misingi ya mazungumzo ya haki na kuheshimiana.


Diplomasia ya kweli haiwezi kujengwa juu ya mashinikizo na masharti ya upande mmoja. Kuitaka Iran iachane na haki zake halali si mazungumzo, bali ni jaribio la kulazimisha,” amesema Araqchi.


Ameongeza kuwa badala ya kujaribu kuudanganya ulimwengu kwa kauli zisizoendana na uhalisia, Marekani inapaswa kurejea katika diplomasia ya kweli na ya heshima, inayozingatia misingi ya usawa wa pande zote na kuheshimu haki za mataifa huru.


Kauli ya Waziri huyo imekuja wakati kukiwa na mjadala mpana wa kimataifa kuhusu mustakabali wa mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Iran na mataifa ya Magharibi, huku Tehran ikisisitiza kuwa haitokubali diplomasia inayokiuka mamlaka na haki zake za kimsingi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha