“Kila mara Israel inaposhindwa kijeshi au inapokabiliwa na shinikizo la kimataifa, hukubali makubaliano ya muda tu ili kupata nafasi ya kujipanga upya na kuendeleza mashambulizi mapya. Hivyo, amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutegemea ahadi zake.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri alitangaza kwamba nchi yake haitaruhusu uhamishaji wa wakaazi wa Gaza kwa hali yoyote, kwa sababu hatua hiyo itakuwa sawa na kufutwa kwa suala la Palestina.