Diplomasia
-
Araghchi: Kujitolea kwa Iran kwa amani na utulivu kunaambatana na diplomasia endelevu na nchi jirani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema dhamira ya Iran ya kudumisha amani na utulivu inaenda sambamba na diplomasia thabiti na endelevu na nchi jirani, akisisitiza umuhimu wa kutafuta suluhisho za kikanda kwa changamoto zinazolikabili eneo.
-
Iran yaonya kuhusu hatua za kuongeza mvutano katika Mlango wa Hormuz iwapo diplomasia itashindikana
Afisa mwandamizi wa Iran amesema kuwa taasisi zote za nchi hiyo zitakuwa tayari kwa uwezekano wa kuongezeka kwa mvutano katika Mlango wa Hormuz na eneo la Mashariki ya Kati iwapo juhudi za kidiplomasia zitashindikana. Wakati huohuo, vyanzo vya kijeshi vya Lebanon vimesema hakuna upanuzi wa maeneo mapya ya majaribio kusini mwa Lebanon wala kuondoka kwa vikosi vya Israel kwa sasa.
-
Meja Jenerali Abdollahi: Uwepo wa Rezaei katika Baraza la Usalama wa Taifa utaimarisha uratibu kati ya uwanja wa vita na diplomasia
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya, Meja Jenerali Ali Abdollahi, amesema uwepo wa Mohsen Rezaei katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika uratibu wa kimkakati kati ya shughuli za uwanjani na diplomasia, pamoja na masuala ya kiusalama, kiuchumi na kisiasa.
-
Kazem Gharibabadi: Diplomasia Haiishii Wakati wa Vita, Bali Hubadilisha Lugha Kulingana na Hali ya Uwanja wa Mapambano
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Sheria na Kimataifa amesema diplomasia huendelea hata wakati wa vita, lakini msimamo na lugha yake lazima viendane na mazingira ya mapambano bila kuonyesha dalili yoyote ya udhaifu mbele ya adui.
-
Wall Street Journal: Trump Arejea Kwenye Diplomasia dhidi ya Iran
Marekani imeelekeza upya mkakati wake dhidi ya Iran kutoka chaguo la kijeshi kwenda kwenye diplomasia, baada ya tathmini kuonyesha kuwa kupata ushindi wa haraka na wa moja kwa moja dhidi ya Iran si jambo rahisi.
-
Mhadhiri wa Sala ya Ijumaa Tehran: Makombora na Diplomasia Vimeimarisha Mizani ya Nguvu kwa Manufaa ya Iran
Mhadhiri / Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema uwezo wa makombora ya Iran pamoja na diplomasia madhubuti ndivyo vilivyoimarisha mizani ya nguvu kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha imani ya wananchi.
-
Iran yashiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Mkataba wa Urafiki na Ushirikiano wa Asia ya Kusini-Mashariki
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Kisiasa na Kimataifa, Saeed Khatibzadeh, ameiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika maadhimisho ya miaka 50 ya Mkataba wa Urafiki na Ushirikiano wa Asia ya Kusini-Mashariki (TAC), yaliyofanyika Manila, Ufilipino.
-
Araghchi: Iran Iliingia Katika Mazungumzo Ili Kuthibitisha Kuwa Marekani na Israel Hawawezi Kujadiliana kwa Uaminifu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa Iran iliingia katika mazungumzo baada ya kutumia njia zote za kidiplomasia, ili kuthibitisha kwamba tatizo halikutokana na kutokuwepo kwa mazungumzo.
-
Pakistan yataka utulivu urejee katika Mlango wa Hormuz, yahimiza mazungumzo badala ya mzozo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesisitiza umuhimu wa kurejea kwa hali ya kawaida katika Mlango wa Hormuz, ikitaka pande zote kujizuia, kulinda usalama wa usafiri wa baharini na kutoa kipaumbele kwa mazungumzo na diplomasia ili kudumisha amani na utulivu wa kikanda.
-
“Diplomasia ya Aya”: Aya za Qur'ani zilizosomwa katika marasimu ya mazishi ya Kiongozi Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei zavutia hisia za wengi
Katika marasimu ya kuuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei (Quds Sirruh), uteuzi wa Aya za Qur'ani Tukufu zilizosomwa kwa kila ujumbe wa wageni waliotoa salamu za rambirambi ulivutia hisia za wengi, huku kila Aya ikionekana kubeba ujumbe maalumu wa kisiasa, kiitikadi na kiroho.
-
Iran na Oman Zasisitiza Kutumia Fursa ya Kidiplomasia Kuimarisha Amani na Usitishaji Vita
Iran na Oman zimesisitiza umuhimu wa kutumia fursa ya sasa ya kidiplomasia kuunga mkono amani, kupunguza mvutano na kuimarisha utulivu kwa kuzingatia sheria za kimataifa na ujirani mwema.
-
Jeshi la Iran: Tuko tayari kutekeleza amri za Kiongozi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na kujibu ukiukaji wowote wa adui
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuwa vikosi vyake vipo katika hali ya utayari wa juu, vikiwa “na mikono kwenye vichocheo vya silaha na masikio yakisubiri amri za Kiongozi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi,” likisisitiza kuwa litailinda Iran na maslahi yake endapo upande wa adui utakiuka makubaliano yaliyofikiwa.
-
Urusi Yapinga Wito wa Kurejesha Ukaguzi wa Nyuklia Iran, Yailaumu Marekani na Washirika Wake
Mwakilishi wa Urusi mjini Vienna amesema wito wa nchi za Magharibi wa kurejesha mara moja ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran hauna uhalali, akieleza kuwa hatua za Marekani na washirika wake ndizo zilizochochea hali ya sasa.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Vikosi vya Iran Havitasita Kuilinda Nchi na Kujibu Uchokozi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amesema matukio ya usiku uliopita yameonyesha wazi kuwa vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kuitetea nchi wakati wowote, huku akiilaumu Marekani kwa kudhoofisha mchakato wa kidiplomasia kupitia ujumbe unaokinzana na ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita.
-
Putin: Iran Haina Nia ya Silaha za Nyuklia, Aunga Mkono Kusitishwa kwa Hatua za Kijeshi
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa Iran haina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia na ina haki ya kutumia urani kwa madhumuni ya amani. Aidha, ameunga mkono kusitishwa kwa hatua za kijeshi akilielezea hilo kuwa ni hatua ya busara kuelekea amani ya kudumu.
-
Ghalibaf: Hatuamini Ahadi za Adui, Kipimo ni Matokeo ya Vitendo
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema kuwa Iran haitategemea ahadi za maadui katika medani ya diplomasia, akisisitiza kuwa mafanikio hupimwa kwa matokeo halisi na kwamba umoja wa wananchi umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha nafasi ya taifa hilo katika kukabiliana na mashinikizo ya nje.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema makubaliano na Marekani yako “karibu kufikiwa”; Trump asema anapendelea diplomasia
Abbas Araghchi amesema makubaliano na Marekani yako karibu kufikiwa ikiwa diplomasia itapewa kipaumbele, huku Donald Trump akisisitiza kuwa anapendelea mazungumzo badala ya vita.
-
Abbas Araghchi: Makubaliano Yanawezekana Ikiwa Diplomasia Itapewa Kipaumbele
Abbas Araghchi amesema kuwa mazungumzo kati ya Iran na Marekani yataanza tena mjini Geneva kwa kuzingatia makubaliano ya awali, akisisitiza kuwa Tehran ina nia ya dhati ya kufikia makubaliano ya haki haraka iwezekanavyo. Ameeleza kuwa Iran haitafuti silaha za nyuklia, lakini haitakubali kunyimwa haki yake ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani, akibainisha kuwa huu ni “wakati wa kihistoria” wa kutatua wasiwasi wa pande zote kupitia diplomasia.
-
-
Ujumbe wa Hongera wa Rais Pezeshkian kwa Kiongozi wa Wakatoliki Duniani
Katika kuendeleza diplomasia ya kidini na kuimarisha maadili ya kuishi kwa amani kati ya wafuasi wa dini mbalimbali, Rais wa Jamhuri alitoa ujumbe rasmi wa pongezi kwa kiongozi wa Wakatoliki duniani, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana, mazungumzo ya kidini na mshikamano wa kibinadamu katika dunia ya leo.
-
Araqchi: Marekani Haitaki Diplomasia ya Kweli, Bali Kulazimisha Iran Kunyimwa Haki Zake
Araqchi: "Diplomasia ya kweli haiwezi kujengwa juu ya mashinikizo na masharti ya upande mmoja. Kuitaka Iran iachane na haki zake halali si mazungumzo, bali ni jaribio la kulazimisha,”