Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jarida la Kijerumani "Focus" limeandika: Mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran hayajazaa matunda, bali yameyumbisha kwa kiasi kikubwa Mfumo wa Kimataifa wa kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia (NPT).
Vituo vilivyolengwa vya Iran vilikuwa chini ya uangalizi wa Shirika la IAEA, ambalo halijawahi kusema kuwa Iran imeamua kutengeneza Bomu la Nyuklia.
Marekani na Israel wametikisa utaratibu wa Dunia ulioanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, kwa kuvunja Mamlaka ya Mataifa, kupuuza Diplomasia, na kurejea kwenye hali ya "Sheria ya Msituni".
Kukua kwa kutokuaminiana kwa Iran dhidi ya Marekani kunaweza kuipeleka Tehran kujihoji upya juu ya mikakati yake ya Nyuklia - Jambo ambalo linaweza kuwa na madhara hatarishi Kimataifa.
Your Comment