IAEA
-
Iran Yapinga Uanachama wa Marekani katika Bodi ya Magavana ya IAEA
Iran yasema uwepo wa Marekani katika Bodi ya Magavana ya IAEA unakinzana na Mkataba wa Wakala huo na kutaka uanachama wa Washington usitishwe.
-
Iran: Baghai Amshutumu Grossi kwa Kudhoofisha Uaminifu wa IAEA
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghai, amemshutumu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, kwa kutumia ripoti za kitaalamu za wakala huo katika muktadha wa kisiasa, akidai kuwa hali hiyo inahatarisha uaminifu, uhuru na kutokuegemea upande wowote kwa taasisi hiyo.
-
Iran, China na Urusi katika Baraza la Magavana la IAEA: Rasimu ya Azimio dhidi ya Iran ni ya Kisiasa na Haina Tija
Iran, China na Urusi zimekosoa rasimu ya azimio dhidi ya Iran katika Baraza la Magavana la IAEA, zikisema ni ya kisiasa na inalenga kuongeza shinikizo badala ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, huku zikisisitiza kuwa hatua hizo zinaweza kuhatarisha diplomasia na utulivu wa nyuklia.
-
Urusi Yapinga Wito wa Kurejesha Ukaguzi wa Nyuklia Iran, Yailaumu Marekani na Washirika Wake
Mwakilishi wa Urusi mjini Vienna amesema wito wa nchi za Magharibi wa kurejesha mara moja ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran hauna uhalali, akieleza kuwa hatua za Marekani na washirika wake ndizo zilizochochea hali ya sasa.
-
Iran Yalaani Azimio la Baraza la Magavana la IAEA, Yasisitiza Itajibu na Kulinda Haki Zake
Ujumbe wa Iran mjini Vienna umesema kuwa azimio la Baraza la Magavana la IAEA dhidi ya Iran ni la kisiasa na lisilo la kitaalamu, ukisisitiza kuwa Tehran itajibu hatua hiyo ili kulinda haki zake zisizoweza kuondolewa.
-
Iran Yaikosoa Rasimu ya Azimio la Marekani katika Baraza la Magavana wa IAEA, Yataja Kuwa ya Kisiasa na ya Uchochezi
Iran imeeleza kuwa rasimu ya azimio iliyowasilishwa na Marekani pamoja na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani katika Baraza la Magavana la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ni ya kisiasa na ya uchochezi, ikidai kuwa inalenga kuhamisha lawama kutoka kwa washambuliaji kwenda kwa mhanga.