upande
-
Pakistan yataka utulivu urejee katika Mlango wa Hormuz, yahimiza mazungumzo badala ya mzozo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesisitiza umuhimu wa kurejea kwa hali ya kawaida katika Mlango wa Hormuz, ikitaka pande zote kujizuia, kulinda usalama wa usafiri wa baharini na kutoa kipaumbele kwa mazungumzo na diplomasia ili kudumisha amani na utulivu wa kikanda.
-
Iran: Marekani Imekiuka Mara Kadhaa Hati ya Maelewano; Tehran Yasisitiza Haitaanzisha Ukiukaji wa Makubaliano
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema Hati ya Maelewano kati ya Tehran na Washington inapitia kipindi cha mgogoro, huku ikiishutumu Marekani kwa kukiuka mara kwa mara masharti ya makubaliano hayo na kuhatarisha usalama wa usafiri wa baharini katika eneo.
-
Iran: Ukiukaji wa Ahadi za Marekani Utakabiliwa na Hatua za Kujibu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema Iran haijaomba mazungumzo na Marekani, akisisitiza kuwa sera ya Jamhuri ya Kiislamu inategemea kanuni ya "ahadi kwa ahadi" na kwamba ukiukaji wowote wa ahadi za Washington utakabiliwa na jibu la Iran.
-
Rais Pezeshkian: Sera za Kivamizi za Utawala wa Kizayuni Ndizo Chanzo cha Ukosefu wa Usalama katika Eneo
Rais Masoud Pezeshkian amesema sera za uchokozi za utawala wa Kizayuni ndizo chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama katika eneo, huku Iran na Serbia zikisisitiza umuhimu wa kuimarisha amani, utulivu na ushirikiano wa pande mbili.
-
Uchambuzi: Mashambulizi ya Beirut na Mvutano Mpya wa Kikanda
Kinachoendelea katika shambulizi la Israel dhidi ya Beirut ni kama ifuatavyo: Mashambulizi ya Israel Kusini mwa Beirut yanaonyesha kuendelea kwa mivutano ya kikanda, huku ukiwepo msisitizo kuwa Muqawama - Upinzani- wa Lebanon (Hezbollah) unaona una uhalali wa kukabiliana na jaribio lolote la adui Israel katika kubadilisha mlingano wa usalama katika nchi ya Lebanon.
-
Kundi la “Hanzala” Latuma Onyo Kali kwa Jeshi la Wanamaji la Marekani, Latishia Majibu Makali
Kundi la mtandao linalojiita “Hanzala” limetoa onyo kali kwa wanamaji wa Jeshi la Wanamaji la Marekani, likiwataka kuwasiliana na familia zao, likidai kuwa makombora yako tayari na likitahadharisha kujibu kwa nguvu iwapo kutatokea uchokozi dhidi ya Iran.
-
Ukosoaji Mkali kwa Msimamo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Kuhusu Gaza: “Kuwa na Tahadhari Kuhusu Unachokisema!”
Katibu Mkuu wa Chama cha Adl na Tanmiyya cha Morocco: “Iwapo ni lazima muwahimize Waisraeli wasionao hali ya kibinadamu kuhusu sisi kueneza maadili ya kuishi kwa pamoja na kuvumiliana, basi hilo ni zuri. Lakini je, mnamfanya vipi wakati wao hawatuoni kama binadamu na mawaziri wao wanasema kuwa sisi ni wanyama walioundwa tu kuhudumia wao?!” Kauli hii inaonyesha hisia za hasira na kushinikizwa kutokana na maneno na sera za baadhi ya viongozi wa Israel, na pia inaashiria hoja ya kisiasa na kimaadili kwamba huwezi kutegemea ushirikiano wa haki na maadili ya kibinadamu ikiwa upande mwingine haukuoni kama binadamu.
-
Mchambuzi wa kisiasa wa Lebanon katika mahojiano na shirika la habari la ABNA amesema:
“Kufanya mazungumzo na Iran ni jambo la lazima kwa Trump / Utayari wa Iran kwa vita unapunguza uwezekano wa kutokea kwa vita”
Wissam Nasif Yassin anaamini kuwa hali bado inaelekea zaidi kwenye suluhisho la mazungumzo lililo imara. Anasema kuwa chaguo la vita haliwezi kuondolewa kabisa, lakini kwa kuzingatia uwezo wa Iran, utayari wake na uungwaji mkono wa wananchi kwa uongozi wa Iran, inaonekana kuwa ni vigumu kwa upande wa pili kuthubutu kutumia chaguo la kijeshi.
-
Mwenyezi Mungu Akiwa Upande Wako, Hakuna Awezaye Kukudhuru
Lengo na makusudio ya kauli hii inayosapoti na Aya hizo Tukufu ni kuondoa hofu moyoni, kwa kutomwogopa yeyote anayenuia kuwa “juu yako” au kukudhuru kwa lolote, kwani Mwenyezi Mungu akiwa pamoja nawe, hakuna mwenye uwezo juu yako isipokuwa kwa idhini Yake.
-
Araqchi: Marekani Haitaki Diplomasia ya Kweli, Bali Kulazimisha Iran Kunyimwa Haki Zake
Araqchi: "Diplomasia ya kweli haiwezi kujengwa juu ya mashinikizo na masharti ya upande mmoja. Kuitaka Iran iachane na haki zake halali si mazungumzo, bali ni jaribio la kulazimisha,”
-
Marafiki wa Ukweli Wako Wengi Zaidi Upande wa Pili | Kifo cha Kishahidi kwao hakileti upweke kwao Bali ni Daraja la kukutana na Msafara wa Waumini
"Katika ugeni hakuna hofu ya upweke; marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.” Kwa maana kwamba: Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, walio tayari kumpokea katika safu yao.
-
Kiongozi wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan:
"|Leo, yeyote ambaye hayuko pamoja na watu wa Gaza, basi hayuko pamoja na Mungu pia"
Kiongozi wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, akisisitiza kuwa Marekani na Israel si wa kuaminika wala si marafiki wa Waislamu, aliongeza: Leo, yeyote ambaye hayuko upande wa watu wa Gaza, basi hayuko upande wa Mungu pia.