Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwenyezi Mungu akiwa upande wako, hakuna awezaye kukudhuru kwa lolote. Aya nyingi za Qur’an Tukufu zinaashiria wazi ukweli huu. Miongoni mwa Aya hizo ni:
﴿إِن يَنصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ﴾
“Ikiwa Mwenyezi Mungu atakusaidieni, basi hakuna yeyote atakayewashinda.”Surat Aal-Imran (3:160)
Aya hii inaendana kikamilifu na kauli isemayo: “Siku zote Mungu akiwa upande wako hakuna atakayekuwa juu yako.”
Aya nyingine inayosisitiza maana hiyo ni:
﴿وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ﴾
“Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu, basi Yeye humtosheleza.”
Surat At-Talaq (65:3).
Kwa maana kwamba: ukiwa na Allah, au Allah akiwa upande wako, hakuna nguvu nyingine inayoweza kukushinda.
Aidha, Mwenyezi Mungu anasema:
﴿إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا﴾
“Hakika Mwenyezi Mungu huwatetea wale wanaoamini.”
Surat Al-Hajj (22:38).
Ulinzi wa Allah (s.w.t) humweka Muumini juu daima, wala si chini.
Na pia Allah anatufundisha:
﴿قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَنَا﴾
“Sema: Haitatupata chochote isipokuwa kile Mwenyezi Mungu alichotuandikia.”
Surat At-Tawbah (9:51).
Funzo lililopo katika Aya hizo Tukufu
Lengo na makusudio ya kauli hii inayosapoti na Aya hizo Tukufu ni kuondoa hofu moyoni, kwa kutomwogopa yeyote anayenuia kuwa “juu yako” au kukudhuru kwa lolote, kwani Mwenyezi Mungu akiwa pamoja nawe, hakuna mwenye uwezo juu yako isipokuwa kwa idhini Yake.

Your Comment