Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (as) yamesema wananchi wa Iran na vikosi vyao vya ulinzi, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na chini ya uongozi wa Amiri Jeshi Mkuu, vimethibitisha kuwa Marekani na Israel hawana njia nyingine isipokuwa kukiri kushindwa na kusalimu amri mbele ya uthabiti wa taifa la Iran.
Lengo na makusudio ya kauli hii inayosapoti na Aya hizo Tukufu ni kuondoa hofu moyoni, kwa kutomwogopa yeyote anayenuia kuwa “juu yako” au kukudhuru kwa lolote, kwani Mwenyezi Mungu akiwa pamoja nawe, hakuna mwenye uwezo juu yako isipokuwa kwa idhini Yake.