Lengo na makusudio ya kauli hii inayosapoti na Aya hizo Tukufu ni kuondoa hofu moyoni, kwa kutomwogopa yeyote anayenuia kuwa “juu yako” au kukudhuru kwa lolote, kwani Mwenyezi Mungu akiwa pamoja nawe, hakuna mwenye uwezo juu yako isipokuwa kwa idhini Yake.
Qur’ani si kitabu cha kusomwa kwa macho na kufahamika kwa fikra pekee. Qur’ani ni minong’ono ya Mola kwa nyoyo zilizo na masikio ya roho. Adabu ya tilawa si sura za nje tu; adabu ya kusoma Qur’ani ni kutambua kuwa umeingia katika uwepo wa Allah, na kwamba kila aya ni pumzi kutoka kwa Mola wa walimwengu, na wewe ndiye unayeambiwa.