Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, “Abu Ubaida”, msemaji mpya wa Brigedi za Al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas), katika hotuba yake ya kina aliyotoa usiku wa leo, mbali na kutangaza kuuawa shahidi kwa baadhi ya makamanda wakubwa wa harakati hiyo, alirejelea operesheni ya “Kimbunga cha Al-Aqsa” ya tarehe 7 Oktoba, akiitaja kuwa ni “mlipuko mzito dhidi ya dhulma, uonevu na mzingiro”.
Aliendelea kusema: “Kimbunga hiki kimerudisha tena suala la Palestina katika kitovu cha uangalizi wa dunia na kuamsha dhamiri za watu huru kote ulimwenguni.”

Akizungumzia suala la usitishaji mapigano na kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza, msemaji huyo mpya wa Al-Qassam alisema: “Usitishaji mapigano na kukoma kwa umwagaji damu Gaza ni matunda ya msimamo thabiti wa watu wetu na ustahimilivu wa wapiganaji wa mapambano.”

Katika kuzungumzia kipindi cha baada ya usitishaji mapigano, alisisitiza: “Licha ya mashambulizi yote na ukiukwaji wa mara kwa mara uliotokea tangu kusitishwa kwa vita, na licha ya mistari yote myekundu ambayo adui ameivuka, mapambano yameendelea kuheshimu ahadi zake na kutenda kwa uwajibikaji kamili, yakizingatia maslahi ya watu wetu.”
Abu Ubaida aliongeza: “Tunataka Israel ivuliwe silaha, na tunasisitiza kwamba taifa la Palestina kamwe halitaweka silaha zake chini, na kwamba juhudi au michakato ya kushughulikia silaha za Wapalestina lazima ikomeshwe.”

Msemaji wa Brigedi za Al-Qassam alionya pia: “Tunasitiza kwamba haki yetu ya kujibu uhalifu wa mvamizi ni haki ya kiasili na iliyohakikishwa. Tunazitaka pande zote husika kuizuia serikali ya Kizayuni na kuilazimisha kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa.”
Hapo Chini ni Picha za Sura Halisi ya Shahidi Abu-Ubaida


Your Comment