29 Desemba 2025 - 22:58
Viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza Watunukiwa Tuzo za Amani Kupitia Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026

Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026 imetoa tuzo za heshima kwa viongozi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Jeshi la Polisi, kama ishara ya kutambua mchango wao katika kudumisha amani, mshikamano na utulivu wa kijamii. Tuzo hizo zilitolewa katika hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za serikali, vyombo vya ulinzi na jamii kwa ujumla kuelekea maandalizi ya tukio hilo muhimu la Maridhiano Day 2026.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026 imetoa tuzo za shukrani kwa viongozi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Jeshi la Polisi, kama kutambua mchango wao katika kudumisha amani, mshikamano na ushirikiano wa kijamii.
Tuzo hizo zilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Mheshimiwa Leila Bhanji, ambaye aliambatana na viongozi wa Jumuiya ya Madhehebu ya Kiislamu Tanzania (JMAT) Kanda ya Ziwa, wakiongozwa na Mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Mwanza.

Viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza Watunukiwa Tuzo za Amani Kupitia Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026


Katika hafla hiyo, tuzo zilikabidhiwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Saidi Mohamed Mtanda, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Wilford Mutafungwa.


Aidha, viongozi hao walitembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, ambapo walipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Omary Mtuwa.


Kamati ya Maandalizi ya Maridhiano Day 2026 imepongezwa kwa juhudi zake kubwa katika maandalizi ya tukio hili muhimu na lenye heshima, linalolenga kuimarisha umoja, amani na mshikamano katika jamii.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha