Mayahudi wanao uchukia Uzayuni huko New York, walihudhuria katika Ofisi ya Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa mjini New York na kutoa heshima zao kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni.
Ofisi ya habari ya Israel imeripoti kuwa, tangu kuanza mashambulizi ya makombora mazito ya Jamhuri ya Kiislamu ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Wazayuni 24 wameuawa na wengine 592 wamejeruhiwa.