16 Juni 2025 - 15:01
Waisraeli 24 wauawa na 592 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Iran katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu

Ofisi ya habari ya Israel imeripoti kuwa, tangu kuanza mashambulizi ya makombora mazito ya Jamhuri ya Kiislamu ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Wazayuni 24 wameuawa na wengine 592 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, kwa mujibu wa tangazo la ofisi ya vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel, tangu kuanza kwa mashambulizi ya makombora ya Iran ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu siku ya Ijumaa, Wazayuni 24 wameangamizwa na watu wasiopungua 592 wamejeruhiwa.

Idhaa ya sauti ya jeshi la Israel imeripoti kuwa, idadi ya wahanga wa Kizayuni katika mashambulizi ya jana usiku ya Iran ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu imefikia 8.

Channel 12 ya Televisheni ya utawala huo ghasibu iliripoti kuwa tangu kuanza kwa operesheni ya "Odeh Sadeq 3", Iran imerusha makombora 370 ya balistiki na zaidi ya ndege 100 zisizo na rubani katika duru 11 za mashambulizi dhidi ya shabaha za utawala huo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha