Kwa miaka mingi, Iran iliwaonya majirani zake wa Kiarabu kuhusu hatari ya kuruhusu Marekani kujenga kambi za kijeshi katika ardhi zao, ikisema uwepo wa majeshi ya kigeni ungeweza kuzifanya nchi hizo kuwa sehemu ya vita dhidi ya Iran. Leo, baada ya kuanza kwa mapambano, kambi hizo zimegeuka kuwa maeneo ya mashambulizi, huku watawala wa Kiarabu wakijikuta wakikabiliwa na matokeo ya maamuzi waliyoyafanya hapo awali.
Watu wengi walipoona kambi nyingi za kijeshi za Marekani zikizunguka Iran, walidhani kuwa Iran haitaweza kujinasua na kwamba kambi hizo zingekuwa sababu ya kuanguka kwake. Hata hivyo, kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu, nguvu, maandalizi na uwezo wa kujilinda ni miongoni mwa misingi muhimu ya kukabiliana na maadui.