“Kila mara Israel inaposhindwa kijeshi au inapokabiliwa na shinikizo la kimataifa, hukubali makubaliano ya muda tu ili kupata nafasi ya kujipanga upya na kuendeleza mashambulizi mapya. Hivyo, amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutegemea ahadi zake.”
Abbas Araqchi alisema: "Tofauti na utawala wa Kizayuni, Iran haitaficha kamwe hasara zake na inajivunia Mashahidi wake kama vielelezo vya ujasiri. Taifa la Iran litasimama kidete dhidi ya yeyote anayejaribu kuliamulia mustakabali wake hadi tone la mwisho la damu".