3 Julai 2025 - 21:51
Bondia Muhammad Ali: "Ikiwa unataka kuuelewa Uislamu, basi kwanza jifunze uelewe tukio la Karbala"

Muhammad Ali - Bondia maarufu wa wakati wote alitoa kauli hiyo mwaka 1993 katika Mwezi kama huu wa Muharram ambapo naye alishiriki katika Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNAMuhammad Ali - Bondia maarufu wa wakati wote alitoa kauli hiyo - kwamba: "Ikiwa unataka kuuelewa Uislamu, basi kwanza jifunze uelewe tukio la Karbala" - Mwaka 1993 katika Mwezi kama huu wa Muharram, ambapo naye alishiriki katika Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as).

Katika picha hiyo hapo juu, Bondia huyu Muhammad Ali, ambaye kwa sasa ni Marehemu, anaonekana akiwa pamoja na Ayatullah Ehsanbaksh wakishiriki katika Maombolezo ya Shahada Imam Hussein (as) katika mwezi wa Muharram, mwaka 1993.

Tukio hili linaonesha kuwa Karbala si tukio la kihistoria tu, bali ni shule ya haki, ujasiri, na mapambano dhidi ya dhulma, inayovuka mipaka ya mataifa na lugha, na kugusa mioyo ya watu wote wanaopenda Ukweli na Haki duniani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha