Ukweli
-
Upole na Huruma ya Mtume Muhammad (saww); Siri ya Kuenea kwa Uislamu
Mtume Muhammad (saww), kupitia tabia yake njema na tukufu, huruma yake isiyo na mipaka, pamoja na subira na uvumilivu wake dhidi ya matendo mabaya aliyofanyiwa, aliwabadilisha maadui wakubwa kuwa marafiki waaminifu. Maadili haya matukufu, ambayo Mwenyezi Mungu ameyasifu kupitia aya: “Na hakika wewe una tabia tukufu kabisa” na “Kwa sababu ya rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu umekuwa mpole kwao”, yalikuwa siri kuu ya kuenea kwa Uislamu duniani. Msamaha wa jumla wakati wa Ushindi wa Makka, kuwatendea mateka kwa heshima na kuwafanyia mema, kuheshimu utu wa mwanadamu hata katika kilele cha uadui, unyenyekevu na maisha ya kawaida licha ya cheo chake cha juu cha Utume, pamoja na huruma yake kwa watoto na wanyonge, vilikuwa miongoni mwa ukamilifu wa maadili yake yaliyotekwa nyoyo za watu na kuvunja safu za wapinzani. Mwenendo huu wa Mtume (saww), uliojaa rehema na huruma na ambao ulikuwa udhihirisho kamili wa “rehema kwa walimwengu”, haukusababisha tu makundi makubwa ya watu kusilimu katika zama za mwanzo za Uislamu, bali utaendelea milele kuwa mfano wa kudumu wa kuwaalika watu kwenye haki na kuangaza njia ya watafuta ukweli.
-
Baqaei: Sera ya Marekani dhidi ya Iran na Kanda Ya Mashariki ya Kati Inategemea Sana Uongo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema sera ya Marekani dhidi ya Iran na eneo hilo inakabiliwa na utegemezi mkubwa wa uongo, akionya kuwa mwenendo huo unaweza kuifanya Marekani ishindwe kutofautisha ukweli na uongo.
-
Wanahabari ni Wasimuliaji wa Ukweli na Mashahidi wa Zama
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA), Hussein Jaberi Ansari, ametembelea mji wa Borujerd katika maadhimisho ya Siku ya Wanahabari nchini Iran, akisisitiza umuhimu wa wanahabari kama wasimuliaji wa ukweli na mashahidi wa matukio ya zama zao.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran:
Mapinduzi ya Kiislamu ni Tunda la Shule ya Ashura, Sayyida Zainab (as) ni Mbeba Bendera ya Jihadi na Ufafanuzi wa Ukweli
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema Mapinduzi ya Kiislamu yamejengwa juu ya misingi ya Ashura, akisisitiza kuwa Sayyida Zainab (as) alichukua nafasi ya kipekee katika kuendeleza ujumbe wa Karbala na kuhifadhi malengo ya mapinduzi ya Imam Hussein (as).
-
Marafiki wa Ukweli Wako Wengi Zaidi Upande wa Pili | Kifo cha Kishahidi kwao hakileti upweke kwao Bali ni Daraja la kukutana na Msafara wa Waumini
"Katika ugeni hakuna hofu ya upweke; marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.” Kwa maana kwamba: Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, walio tayari kumpokea katika safu yao.
-
Jeshi la Lebanon liliwaruhusu waandishi wa habari kuingia katika vituo vya Hizbullah;
JKituo cha kihistoria cha Muqawama ambacho ukweli wake umejulikana baada ya kusitishwa kwa mapigano
Bonde la Zabqin, kutokana na muundo wake maalum wa kijiografia na umbali wa takribani kilomita 10 kutoka mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, linachukuliwa kuwa mojawapo ya ngome kuu za Muqawama (Upinzani). Ni ngome ambayo vizazi mbalimbali vya wapiganaji wa Kipalestina na Wenyeji wa Lebanon wamekuwa wakikuwapo humo kwa miaka mingi.