Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA -, Ayatollah Mohsen Faqihi, Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom, amefanya ziara katika Ofisi ya Wahariri ya Shirika la Habari la Kimataifa la ABNA katika Mji wa Qom mida ya alasiri ya leo, Jumatano, Aprili 09, 2025, ili kufahamishwa kuhusiana na shughuli mbalimbali za Shirika hili la Habari.
Kufuatia ziara hii, Ayatollah Faqihi alionekana akiwa sambamba na Waandishi wa Habari kutoka katika Shirika la Habari la ABNA na, katika hotuba yake, alielezea dhamira ya vyombo vya Habari katika hali ya sasa na umuhimu wa kuchunga Maadili ya Vyombo vya Habari katika upashaji na utoaji wa Habari.
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom, katika hotuba ya kuthamini huduma za Shirika la Habari la ABNA, aliwahutubia Waandishi wa Shirika la Habari la ABNA na kusema: Shirika la Habari la ABNA hutoa huduma zinazostahili katika lugha tofauti, na huduma hizi zinastahili kuthaminiwa, kupongezwa na kushukuriwa. Shakhsia kubwa wanafanya kazi katika Shirika la Habari la ABNA, na Mwenyezi Mungu akipenda (Insha Allah), wapendwa hawa wote watapata Taufiq ya Mwenyezi na kufanikiwa.
Nyinyi, waheshimiwa, nyote ni wanamapinduzi na wafuasi wa Wilayat Al-Faqih, na kutimiza wajibu wenu wa kidini ndiyo heshima kuu na adhimu tunayoweza kuwa nayo. Hivyo, ni lazima tuwe na nia ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu katika kazi yetu. Tukifanya hivyo kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, basi kwa hakika kheri za dunia na akhera zitaandikwa kwa ajili yetu.
Akaendelea kusema: Imam Sadiq (AS) alisema katika riwaya ijulikanayo kwa jina la Basri kwamba ukweli / uhakika wa uja upo katika mambo makuu matatu. Kwanza ni kwamba mtu anapaswa kuzingatia ukweli kwamba chochote alicho nacho kimetoka kwa Mwenyezi Mungu. Sisi kama Wanadamu, ikiwa tuna hadhi, uzuri, au mali n.k, yote hayo yametolewa (tumepewa) na Mwenyezi Mungu. Hivyo ni lazima tujue kwamba sifa zozote tulizo nazo zinatoka kwa Mwenyezi Mungu na tufaidike na sifa hizo katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana kwamba: Utajiri, uzuri, na hadhi n.k, yote hayo ni ya Mwenyezi Mungu, na lazima tuyatumie katika njia ya kiungu, na ikiwa tutaweza kufanya hivyo, basi huo ndio ukweli na uhakika wa uja wa mja.
Imam (a.s) anasema: "(العبدُ و ما فی یده کانَ لِمولاه) / "Mtumwa (Mja), yeye mwenyewe na mali yake, wote ni mali ya Bwana wake (Mwenyezi Mungu)." Jambo la pili ni kwamba lazima tujue kwamba usimamizi wa mambo uko mikononi mwa Mungu. Wanadamu wana wajibu wa kutekeleza amri za Mungu na kuacha makatazo ya Mungu, lakini wanapaswa kujua kwamba usimamizi wa mambo uko mikononi mwa Mungu, na hili likitupata, misiba itakuwa rahisi kwetu.
Jambo la pili ni kwamba: Lazima tujue kwamba usimamizi wa mambo uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Wanadamu wana wajibu wa kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu na kuacha makatazo ya Mwenyezi Mungu, lakini pia wanapaswa kujua kwamba usimamizi wa mambo yote uko Mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na ikiwa tutalitambua hilo na kuwa katika hali hiyo, basi kwa hakika misiba (matatizo, mabalaa, majaribu na misukosuko) itakuwa rahisi sana kwetu.
Ayatollah Faqihi amesema kuwa Imam Khomeini (RA) alikuwa mvumilivu wakati wa mkasa (msiba) wa kuuawa Shahidi Ayatollah Sayyid Mustafa Khomeini (RA) na kuongeza: "Wakati fulani, misiba inatokana na neema ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuzingatia suala hili, hurahisisha (hufanya kuwa ni rahisi mno) kulibeba janga hilo."
Mwanachama (Mjumbe) huyu wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom alibainisha akisema: “Jambo la tatu ni kwamba ni lazima tujishughulishe na kazi moja katika maisha yetu yote, kuanzia mwanzo wa kazi yetu hadi wakati wa kifo chetu, nayo ni kazi ya kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu na kuacha makatazo ya Mwenyezi Mungu. Kila neno tunaloandika lazima liwe la kumpendeza Mwenyezi Mungu na Imam wa Zama (a.t.f.s). Maneno yetu, hotuba zetu, hatua zetu, na kila jambo tunalofanya lazima liwe la kumpendeza Mwenyezi Mungu (na kutufanya tuwe ni wenye kuchuma radhi Zake). Sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu, hivyo tuhakikishe daima kuwa matendo yetu yote ni yenye kumpendeza Imam wa Zama (a.t.f.s) na Mwenyezi Mungu, vinginevyo tutakuwa ni waja wa mali na vyeo. Na kwa kuwa sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu, basi kwa hakika mawazo yetu, matendo yetu, na maandishi (maandiko) yetu yote yatakuwa ni kwa ajili ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Aidha alisema kwamba: “Mashirika ya Habari yakiwa na unyoofu, ukweli na uaminifu, na yakiacha masuala ya kando kando, na kutafuta ukweli na uhakika, basi kwa hakika matatizo mengi yatatatuliwa.” Tatizo letu, kama alivyosisitiza Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, ni kukosa maafisa wakujitolea na waliobobea.
Nchi yetu ina uwezo mkubwa katika suala la migodi, rasilimali za chini ya ardhi, na utajiri. Hivyo, ni lazima tuwe nchi bora zaidi ulimwenguni, na hii inahitaji Mtaalam (Afisa) wa kujitolea (kwa moyo mkunjufu). Mashirika ya Habari yanaweza kumtengeneza na kumsahihisha Afisa kama huyo, na kumuwajibisha Afisa huyo, na kwa njia hiyo mambo yatarekebishwa.
Hassan Sadraei Aref, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la ABNA, alisema mwanzoni mwa ziara hii kwamba Shirika la Habari linafanya kazi katika lugha 27, na kuongeza: "Hakuna eneo duniani ambalo watu wa eneo hilo hawazungumzi mojawapo ya lugha zinazopatikana katika Shirika la Habari la ABNA."
Chombo hiki cha Habari kinazingatia elimu na maarifa ya Kishia na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), pamoja na matukio ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s). Kufanya hafla ya Ghadir katika Mji wa Igdir, Türkiye, pamoja na kushikilia duru za mashairi pamoja na kuwepo kwa washairi wa Ahlu al-Bayt (a.s) kutoka nchi tofauti tofauti, ni miongoni mwa mipango mingine iliyochukuliwa na Shirika la Habari la ABNA.
Your Comment