Hii ni tafsiri muhimu inayoonyesha kuwa ushuhuda wa imani unaonyeshwa kivitendo, si kwa historia au usuhuba wa Mtu kwa Mtume au kuishi Zama moja na Mtume (saww).
Akiashiria umuhimu wa ukweli na uaminifu katika vyombo vya habari, Ayatollah Faqihi alisema: "Ikiwa tutadumisha ukweli na uaminifu katika uwanja wa taarifa na usambazaji wa habari, basi kwa hakika tunaweza kutoa huduma kubwa katika uwanja huu."