Mafundisho
-
Mkuu wa Mahusiano ya Kigeni wa Hizbullah ya Lebanon: Umoja wa Kiislamu ni dhamana ya ushindi wa Umma dhidi ya utawala wa Kizayuni
Mkuu wa Mahusiano ya Kigeni na Mjumbe wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi umoja wa Kiislamu na kufuata mafundisho ya Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) kuhusu huruma na uongofu, akieleza juu ya juhudi endelevu za maadui katika kuharibu sura ya Uislamu.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Kuwasaidia Wapalestina Wanaodhulumiwa Ni Wajibu wa Mataifa ya Kiislamu
"Mara tu matatizo ya Waislamu yanapoanza, basi hilo huwa ni matokeo ya kugeuka mbali na Qur’an na mwongozo wa Mtume. Suluhisho la kweli ni kurejesha uhusiano wa dhati na Qur’an na Sunnah ya Mtume (s.a.w.w).”
-
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Kidini katika masuala ya Hija na Ziara:
"Kufuata mtindo wa maisha wa Imam Hussein (a.s) ni suluhisho kwa changamoto za jamii ya leo"
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Kidini katika Masuala ya Hija na Ziara, katika hafla ya kufunga tukio la pili la kimataifa la vyombo vya habari “Nahnu Abna’ Al-Husayn (a.s)”, alisisitiza umuhimu wa kunufaika na mtindo wa maisha na mafundisho ya Imam Husayn (a.s) ili kujibu mahitaji ya jamii ya leo.
-
Dkt. Pezeshkian: Umoja na Mshikamano Nguvu Yetu Dhidi ya Maadui
Alionya dhidi ya kuvunjika kwa mshikamano wa taifa na urafiki wa majirani, akibainisha kuwa hayo ni malengo ya Marekani na Israel ya kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu na nchi za jirani.
-
Katika Kumbukizi ya Imam Reza (a.s): Kiongozi Mkuu Atoa Wito wa Kulinda Umoja na Kukemea Jinai za Kizayuni
Ayatollah Khamenei: "Marekani Haitaki Iran Isimame Imara, Bali Itii Amri Zake".
-
Falsafa ya ‘Iddil Hajj (Eid al-Adha) kwa Mtazamo wa Ahlul Bayt (a.s)
Eid al-Adha ni zaidi ya kusherehekea; ni ishara ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa moyo wote, kujenga jamii ya huruma na mshikamano, na kuhuisha roho ya kujitolea. Ni nafasi ya kila Mwislamu kujiangalia upya na kuimarisha uhusiano wake na Muumba na viumbe wenzake.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji: "Ulimwengu wa Kiislamu wahitaji kutekeleza mafundisho ya Hija ili kusitisha maafa ya Gaza"
Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Ulimwengu wa Kiislamu kwa sasa unayahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote mafundisho ya Hija, na akibainisha kuwa Hija ya mwaka huu ni msimu wa pili unaofanyika sambamba na jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza, ameuliza swali lifuatalo:“Ni nani anapaswa kusimama dhidi ya janga hili la kibinadamu?” Kisha ameongeza kwa kusisitiza: “Bila shaka yoyote, serikali za Kiislamu ndizo zinazobeba wajibu wa kwanza wa jukumu hili, na mataifa ya Kiislamu yana haki ya kudai utekelezaji wa wajibu huo kutoka kwa serikali zao.”