Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ripoti hii inaonyesha hali ya vyombo vya habari na jinsi vyombo fulani vinavyoweza kutumia mbinu za propaganda kwa lengo la kuathiri mtazamo wa umma.
Katika muktadha huu, Iran International, imekuwa na mchango mkubwa katika kueneza hofu na udhaifu kuhusu hali ya Iran, hasa wakati wa shambulizi la hivi karibuni la Israel dhidi ya Iran.
"Iran International" ambayo inatumika na Utawala haram wa Kizayuni ili kueneza propaganda dhidi ya Iran, ilijikita katika kuonyesha nguvu za Israel na kupunguza morali ya wananchi wa Iran kwa njia ya maudhui na vipindi vilivyohusiana na hofu.
Wananchi wengi wa wa Iran wameamua kuikataa na kuipuuza Televiaheni hiyo.
Badala yake, Television ya "BBC Farsi" sasa inachukua nafasi ya "Iran International" kwa ajili ya kuendeleza mtindo huo huo lakini kwa kutumia njia na mbinu tofauti zaidi, ikiwa na lengo sawa la kuharibu usalama wa ndani na mshikamano wa jamii ya Kiiran.
Propaganda za vyombo vya habari vya kimataifa kama hivi vinavyotumiwa na Wazayuni, unalenga kuleta mgawanyiko na kutengeneza hali ya kutoaminiana ndani ya jamii husika.
Athari za Vyombo vya Habari Vya Propaganda chafu kama hivyo ni:
1. Kupandikiza Hofu na Shaka: Vyombo vya habari vinavyotumika kutengeneza picha mbaya ya serikali au jamii fulani vinaweza kuathiri hali ya usalama na kuleta shaka miongoni mwa wananchi. Hii inaweza kuongeza mivutano na kutoelewana ndani ya jamii.
2. Kushusha Hadharani Hadhi ya Uongozi wa Taifa: Kupitia propaganda, vyombo vya habari vinaweza kupunguza uungaji mkono wa watu kwa Serikali, kwa kuonyesha udhaifu wake au kwa kupotosha ukweli kuhusu hatua za kiusalama na kijeshi.
3. Kueneza Mgawanyiko: Vyombo vya habari vya kimataifa vinavyohusiana na masuala ya kisiasa ya taifa fulani vinaweza kutengeneza mgawanyiko katika jamii, na kusababisha watu kuwa na mtazamo mbaya kuhusu Serikali zao au hata kuhusu wanajamii wenzao.
Je, Vyombo vya Habari vina Wajibu Gani Katika Matukio kama Haya?
Vyombo vya habari vina jukumu muhimu katika kutoa taarifa sahihi na za haki kwa umma.
Ingawa ni haki yao kutoa mtazamo wao, wanapaswa pia kuwa waangalifu kuhusu madhara ya propaganda na jinsi wanavyoweza kuathiri hali ya kisiasa na kijamii.
Katika dunia ya sasa, ni vigumu kujua ukweli kamili kwa urahisi, hivyo ni muhimu kuwa na vyombo vya habari vya kuaminika vinavyotumia vyanzo vya haki na kuthibitisha taarifa kabla ya kuzisambaza. Hivyo ndio Vyombo vya kufuatilia na kusikiliza. Na sio kufuata kila chombo cha Habari bila kujua kuwa hiki chombo kinatumiwa na waovu wa uistikbari wa Dunia au la.
Your Comment