Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Televisheni ya Kizayuni (chaneli ya 12) imeripoti kuwa Mohammad Ali Jamoul, mmoja wa Makamanda wa Kikosi cha Makombora cha Hizbullah, ameuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani (droni) Kusini mwa Lebanon.
Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni alidai kuwa wanajeshi wa Israel leo alfajiri walimshambulia kwa drone gari la Mohammad Ali Jamoul katika mji wa Deir al-Zahrani kusini mwa Lebanon, na kumuua Shahidi.
Vyanzo vya Lebanon pia vimethibitisha kuwa shahidi Jamoul, mwenye umri wa miaka 33, alikuwa anaelekea msikitini kwa ajili ya Swala ya Alfajiri kwa kutumia gari lake binafsi alipolengwa na droni ya jeshi la Israel katika barabara ya Deir al-Zahrani kuelekea Nabatieh, karibu na daraja la waenda kwa miguu.
Kwa mujibu wa televisheni ya chaneli 12 ya Kizayuni, msemaji wa jeshi hilo alidai kuwa Jamoul alikuwa na mchango mkubwa katika mashambulizi dhidi ya vikosi vya Israel wakati wa vita, akihusika na mashambulizi mengi ya makombora dhidi ya ngome za maadui.
Hizbullah Lebanon imethibitisha rasmi kuwa Mohammad Ali Jamoul ameuliwa shahidi kwa mkono wa Israel katika mji wa Deir al-Zahrani.
Hili linatajwa kuwa ni shambulio la kwanza la Israel kufika katika eneo hilo la ndani ya Lebanon, jambo linalochukuliwa kama ukiukwaji wa wazi wa mamlaka ya kitaifa ya Lebanon.
Shahidi Mohammad Ali Jamoul alikuwa anatoka katika familia ya muqawama (upinzani), na kaka yake alishawahi kuuawa shahidi katika mapigano ya Yuhmor al-Shaqif wakati wa vita vya siku 66 dhidi ya uvamizi wa hivi karibuni wa Israel dhidi ya Lebanon.
Your Comment