Mohammad
-
Mwanazuoni wa Kisunni na Imamu wa Swala ya Ijumaa Auawa Shahidi katika Shambulio la Kigaidi Kusini-Mashariki mwa Iran
Mwanazuoni wa Kisunni na Imamu wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ali Ibn Abi Talib, Molavi Mohammad Anwar Rigi, ameuawa Shahidi baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana katika mji wa Mirjaveh, kusini-mashariki mwa Iran. Mamlaka za eneo hilo zimesema uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wa shambulio hilo, huku wananchi wakitakiwa kudumisha utulivu na kutoruhusu tukio hilo kuchochea migawanyiko ya kidini.
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi: Iran Ipo Mstari wa Mbele wa Mhimili wa Muqawama
Hujjatul-Islam Mohammad Taqi Vakilpour amesema Iran ipo mstari wa mbele wa mhimili wa muqawama pamoja na Lebanon, Palestina na Yemen, huku akisisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa, kuimarisha mfumo wa Kiislamu na kukabiliana na juhudi za maadui za kueneza migawanyiko ndani ya jamii.
-
Balozi wa Iran Nchini Iraq Akutana na Patriarki (Baba-Kiongozi) Mpya wa Kanisa la Kaldania, Wasisitiza Umuhimu wa Maelewano na Mshikamano
Balozi wa Iran nchini Iraq, Mohammad Kazem Al-Sadeq, amekutana na Patriarki (Baba-Kiongozi) mpya wa Kanisa la Kaldania, Mar Paulus III Nona, jijini Baghdad ambapo pande hizo zimesisitiza umuhimu wa kuimarisha maelewano ya kijamii, kuishi kwa amani kati ya dini mbalimbali na kuendeleza ushirikiano wa kikanda.
-
Shahidi aliyekuwa akiishi kwa Mashahidi | Simulizi la Mama wa Shahidi kuhusu wakati wa mlipuko na Shahada
moja kwa mzaha nilimwambia mwanangu “Mwanangu! Kwa nini unanibana sana kuhusu kusali kwa wakati?” Alitabasamu na kusema: «Mama! Ninaogopa tufariki bila kusali kwa wakati na tusipate nafasi ya kurekebisha...»