Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, ameidhinisha kuendelea kwa jukumu la Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shahriari kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.
Uamuzi huu umetolewa kufuatia barua kutoka kwa Bw. Mawlana Ishaq Madani, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya hiyo, aliyomwandikia Kiongozi wa Mapinduzi. Barua hiyo iliambatana na ripoti ya kikao cha Baraza Kuu cha Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu, ambapo wengi wa wajumbe walikubali kuendelea kwa Hujjatul-Islam Shahriari kwa muhula mwingine.
Kwa msingi huo, Ayatollah Khamenei amekubali rasmi kuendelea kwa Hujjatul-Islam Shahriari katika wadhifa wake kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.
Your Comment