Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, Hujjatul-Islam Hamid Shahriari, amesema kuwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, alikuwa akiutazama umoja wa Umma wa Kiislamu kama mkakati wa msingi wa kukabiliana na ubeberu, uistikbari na njama za maadui za kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu.
Kiongozi wa Mapinduzi ameidhinisha kuongezwa kwa muda wa jukumu la Hujjatul-Islam Shahriari kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu