Muda
-
Katika mazungumzo ya simu kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Pakistan:
Araghchi alisema: “Azimio namba 2231 la Baraza la Usalama linapaswa kuchukuliwa kuwa limekamilika na kuhitimishwa kwa wakati uliopangwa.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, huku akishukuru msimamo wa uwajibikaji wa Pakistan katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kupinga matumizi mabaya ya nchi tatu za Ulaya, alisisitiza kwamba Azimio namba 2231 lazima, kwa mujibu wa masharti yake na maandiko ya makubaliano ya nyuklia (JCPOA), lichukuliwe kuwa limekamilika katika muda uliopangwa, yaani tarehe 26 Mehr 1404 (18 Oktoba 2025).
-
Maneno Mafupi, Yenye Maana Pana:
Hotuba ya 21 ya Nahjul Balagha: "Kuwa na mzigo mwepesi ili mfike (kwenye safari yenu)!"
تَخَفَّفُوا تَلْحَقُوا، فَإِنَّمَا يُنْتَظَرُ بِأَوَّلِكُمْ آخِرُكُمْ "Punguzeni mizigo ili mfike (kwenye malengo ya safari yenu), kwa maana waliotangulia wanawasubiri mlio nyuma." Hotuba ya 21 ya Nahjul Balagha – Mtazamo wa Akhera katika Jitihada za Binadamu: Hotuba ya 21 ya Nahjul Balagha inaangazia maisha ya binadamu kwa mtazamo wa akhera, na inaeleza kwamba: Binadamu anapaswa kuwa mwepesi wa mizigo (wa kidunia), ili aweze kwa urahisi kutoka duniani na kuelekea kwenye maisha ya akhera. Hili linaonyesha kuwa jitihada za binadamu si kwa ajili ya dunia pekee, bali kwa ajili ya ukamilifu wa kiutu (kamilifu) na maisha ya milele.
-
Kuongezwa kwa muda wa uteuzi wa Majukumu ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu
Kiongozi wa Mapinduzi ameidhinisha kuongezwa kwa muda wa jukumu la Hujjatul-Islam Shahriari kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu
-
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa jukumu la UNIFIL nchini Lebanon hadi mwisho wa mwaka 2026.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuongeza muda wa jukumu la wanajeshi wa UNIFIL kusini mwa Lebanon kwa mara ya mwisho.
-
Abu Muhammad al-Jolani Kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Huku Akiwa Chini ya Vikwazo
Ahmad al-Sharaa, maarufu kama Abu Muhammad al-Jolani, Rais wa Serikali ya Muda ya Syria, anatarajiwa kushiriki na kutoa hotuba katika kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York katika wiki chache zijazo.
-
Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Yaadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) kwa Majlisi Maalum ya Maombolezo
Kikao hicho kilipambwa kwa kisomo cha Qur’an Tukufu na mashairi ya maombolezo (marsiya), ambapo walimu na wanafunzi walishiriki kwa unyenyekevu na hisia za heshima kwa mashahidi wa Karbala.
-
Sudan Kusini na Israel: Ushirikiano wa Kistratejia au Mgongano wa Maslahi?
Kwa ziara rasmi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini nchini Israel, uhusiano wa muda mrefu lakini wa kimya wa mataifa haya mawili umeingia katika hatua mpya.
-
Nafasi ya Maadili ya Kiroho na Ibada katika Malezi ya Kizazi Chenye Mafanikio
Hata kama mtu atatumia saa zote za maisha yake kuwahudumia waja wa Mwenyezi Mungu, bado hawezi kuepuka kuhitajia saa moja kwa ajili ya nafsi yake.
-
Hadithi ya Shetani na Mwanadamu:
"Siri ya Muda wa Shetani Kuishi: Kwa Nini Mwenyezi Mungu Alimpa Shetani Muda Mrefu wa Kuishi?
Tangu wakati huo ambapo Shetani aliasi na kukataa kumsujudia Adam (a.s), mzozo wa kihistoria kati yake na Mwanadamu ulianza; mzozo ambao unaendelea hadi leo hii. Lakini swali muhimu ni hili: Kwa nini Mwenyezi Mungu alimpa adui huyu katili (Shetani) muda mrefu wa kuendelea kuishi na kujaribu na kuwapoteza watoto wa Adam (Wanadamu)?!. Nakuletea Hadithi nzuri na yenye mazingitio ndani yake kuhusu Shetani na Mwanadamu, na utaijua sababu na siri ya Ruhusa ya Mwenyezi Mungu kwa Shetani ili aendelee kuishi kwa muda mrefu.