21 Agosti 2025 - 09:49
Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Yaadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) kwa Majlisi Maalum ya Maombolezo

Kikao hicho kilipambwa kwa kisomo cha Qur’an Tukufu na mashairi ya maombolezo (marsiya), ambapo walimu na wanafunzi walishiriki kwa unyenyekevu na hisia za heshima kwa mashahidi wa Karbala.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Hawza ya Kidini ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) - Iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam Leo (Jumanne: 19 -08- 2025) imeandaa kikao maalum cha maombolezo na kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), tukio lililohudhuriwa na walimu, wanafunzi na waumini kutoka maeneo mbalimbali.

Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Yaadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) kwa Majlisi Maalum ya Maombolezo

Mkutano huu uliofanyika baada ya Sala ya Dhuhraini ulidumu kwa muda wa nusu saa, ambapo hotuba kuu ziliwasilishwa na Mwalimu heshimika, Molana Arif, pamoja na Sheikh Me'raj.

Katika mawaidha yao, wazungumzaji waligusia:

  • Umuhimu wa Arubaini kama ishara ya kudumu ya harakati ya Imam Hussein (a.s) na mapambano dhidi ya dhulma na ukandamizaji.
  • Mchango wa Karbala katika kuamsha dhamiri za waumini na kizazi baada ya kizazi.
  • Wajibu wa vijana na wanafunzi wa madrasa kuendeleza utamaduni wa kushikamana na Qur’an, Ahlul-Bayt (a.s) na misingi ya uadilifu.
  • Umuhimu wa kusoma historia ya Karbala kwa mtazamo wa kiroho na kijamii ili kuhamasisha mabadiliko ya maisha ya kila siku.

Kikao hicho kilipambwa kwa recitation ya Qur’an Tukufu na mashairi ya maombolezo (marsiya), ambapo walimu na wanafunzi walishiriki kwa unyenyekevu na hisia za heshima kwa mashahidi wa Karbala.

Mwisho wa hafla, dua maalum ilitolewa kwa ajili ya kudumisha umoja wa Waislamu, kuondoka kwa dhulma duniani na baraka kwa wanafunzi wote wanaojitolea kujifunza Qur’an Tukufu na mafundisho Matukufu ya Ahlul-Bayt (as).

Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Yaadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) kwa Majlisi Maalum ya Maombolezo

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha