Hawza
-
Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kwa mkutano wa kumbukumbu ya miaka mia moja (100) ya kuanzishwa upya kwa Chuo cha Dini cha Qom:
Ayatollah Khamenei: Jukumu la (Hawza) Chuo cha Kidini ni Kuchora Mipaka Mikuu na Midogo ya Ustaarabu mpya wa Kiislamu
"Kazi kuu na ya msingi ya Hawza ni (البَلاغُ المُبین) kufikisha ujumbe wa dini kwa uwazi na ufasaha (ubalighi wa wazi - Kwa maana: Kufikisha ujumbe kwa uwazi na uthabiti na kwa namna ambayo haiachi shaka yoyote -). Miongoni mwa vielelezo vyake muhimu kabisa ni kuchora na kueleza kwa uwazi mistari (mipaka) mikuu na ya kando ( au midogo) ya ustaarabu mpya wa Kiislamu, pamoja na kuifafanua, kuieneza, na kuikuza katika jamii kama sehemu ya utamaduni."
-
Hawzat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Dar-es-salaam | Wanawake katika Kuadhimisha Shahadat ya Imam Sadiq (a.s) + Picha
Wanawake katika jamii za Kiislamu wanachukua jukumu muhimu katika kuadhimisha kifo cha Kishahidi cha Imam Sadiq (a.s), ambapo si tu wanahudhuria kimwili katika vikao kama hivi vya Maombolezo, bali pia wanashiriki kikamilifu kwa njia ya vitendo katika kueneza mafundisho ya Imam Sadiq (as) katika nyanja mbalimbali.
-
Majukumu ya Mwanalimu na Mwanafunzi (1)
Majukumu ya Mwalimu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu :- Majukumu yake binafsi, majukumu juu ya wanafunzi wake, na majukumu yake akiwa darasani.
-
Siku ya Quds Duniani:
Kongamano la Siku ya Quds Duniani lilifanyika Jijini Tanga, Tanzania
Kuna umuhimu Mkubwa kwa Waislamu na Watu wote huru na wapenda Haki Duniani, kuzidi kusimama pamoja na wadhulumiwa wa Palestina na kutetea Haki za watu wote wanyonge popote pale walipo Duniani. Watu mbalimbali kutoka Jiji la Tanga walihudhuria katika Mkusanyiko huu wa kuhuisha Siku ya Kimataifa ya Quds, wakiwemo Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kidini na Madhehebu mbalimbali.