Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) —ABNA— Kufuatia kifo cha Ustadh Mahmoud Farshchian, Ayatollah Sayyid Hashim Husseini Bushehri, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, alitoa ujumbe wa rambirambi kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Natoa salamu za rambirambi kwa wananchi wote wa Iran na jamii ya sanaa nchini kufuatia kifo cha Ustadh Mahmoud Farshchian, mchoraji maarufu kutoka Isfahan na mmoja wa sura mashuhuri zaidi katika sanaa ya uchoraji wa Kifarsi.
Marehemu aliweka kipaji chake cha kipekee katika kuhudumia thamani na mafundisho ya kidini na kiroho, na kupitia uchoraji wa mchoro maarufu "Asr-e Ashura" (Saa ya Ashura) pamoja na mchoro wa kaburi tukufu la Imam Ridha (a.s) — ambavyo ni miongoni mwa kazi za sanaa za kudumu zaidi katika historia ya Iran — alionyesha kina cha mapenzi na heshima yake kwa thamani za Mwenyezi Mungu.
Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe rehema na maghfira huyu gwiji wa sanaa ya Kiislamu-Kiirani, na awape subira na ujira wote wa familia, jamaa, wanafunzi na wapenzi wa marehemu.
Sayyid Hashim Husseini Bushehri
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom.
Your Comment