Rambirambi
-
Ujumbe wa Rambirambi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Ayatollah Sistani kufuatia Kifo cha Mke Wake
Kufuatia kifo cha mke wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, alituma ujumbe wa rambirambi kwa Marja’ huyu mkubwa.
-
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) kufuatia kifo cha Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi
Kufuatia kifo cha Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi, mkuu wa ofisi ya masuala ya kifedha ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) alitoa ujumbe wa rambirambi.
-
Ujumbe wa rambirambi wa Ayatollah Faqihi kwa mnasaba wa kufariki kwa Ayatollah Mousavi Yazdi
Ayatollah Mohsen Faqihi ametuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Mali (Wujuhat) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
-
Salam za Rambirambi za Baraza la Maulamaa na Wenye Mamlaka wa Madhhebu ya Shia nchini Afghanistan Kufuatia Tetemeko la Ardhi Mashariki mwa Afghanistan
Baraza la Maulamaa na Watu Wenye Mamlaka wa Madhehebu ya Shia nchini Afghanistan, kupitia taarifa rasmi, limeeleza masikitiko na mshikamano wao na familia za waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni katika mkoa wa Kunar, mashariki mwa Afghanistan, huku likisisitiza umoja wa kitaifa na hitajio la msaada wa haraka kwa waathirika.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu atoa rambirambi kufuatia kifo cha Msanii wa Kiirani Mahmoud Farshchian: "Ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika"
"Msanii mashuhuri na maarufu, Bwana Mahmoud Farshchian, alikuwa nyota angavu katika anga ya sanaa ya Kiirani. Uaminifu wake na ucha Mungu wake vilimuwezesha kuutumia uwezo wake wa kipekee katika kuhudumia maarifa na mambo ya kidini, na ameacha nyuma kazi za sanaa zisizofutika. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Nawasilisha rambirambi za dhati kwa familia yake, marafiki zake, wanafunzi wake, na jamii ya wasanii nchini."
-
Kiongozi wa Mapinduzi Aomboleza Kifo cha Hujjatul-Islam Naeim Abadi
Mheshimiwa Ayatollah Khamenei ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanazuoni mpiganiaji, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Gholamali Naeim Abadi.
-
Mufti wa Oman:
“Inasikitisha kuwa waandishi wa habari wanauawa Gaza na baadhi wanaendelea kuwaunga mkono wavamizi”
Mufti wa Oman amelaani mauaji ya waandishi wa habari katika mji wa Gaza yaliyofanywa na jeshi la Israel, na kutamka masikitiko yake juu ya kuendelea kwa baadhi ya watu na nchi kuunga mkono wavamizi.
-
Ujumbe wa Rambirambi wa Ayatollah Husseini Bushehri Kufuatia Kifo cha Ustadh Mahmoud Farshchian
Rais wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ustadh Mahmoud Farshchian.
-
Tanzania Yaomboleza Kifo cha Spika Mstaafu Mhe. Job Yustino Ndugai
Katika salamu za rambirambi, pole zimetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla.