Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Kufuatia kifo cha Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi, mmoja wa wanafunzi wa maulamaa wakubwa kama Ayatollah Boroujerdi na Imam Khomeini (qdd), na aliyekuwa mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Kifedha ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) alitoa ujumbe wa rambirambi uliowasilishwa kwa mwanawe marehemu.
Matni wa Ujumbe wa Ayatollah "Reza Ramadhani" ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika sisi kwake tutarejea."
Mheshimiwa Hujjatul Islam wal-Muslimin Bwana Hajj Sayyid Mohsen Mousavi Yazdi (hifadhiwe izza yake),
Assalamu alaykum bima ṣabartum (Amani iwe juu yenu kwa yale mliyovumilia),
Habari za kufariki kwa baba yako mpendwa, Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi (raḥmatullāhi 'alayh), imenisikitisha sana na kunihuzunisha.
Mwanazuoni huyo wa kiroho, mwenye tabia njema, alitumia maisha yake matukufu kwa ajili ya kuhifadhi na kusambaza mafundisho ya Qur'ani Tukufu na AhlulBayt (a.s), pamoja na kuhudumia seminari za kielimu, Imam wawili wa Mapinduzi, wanazuoni wakuu wa kidini, wanafunzi wa elimu ya dini, na watu waumini walioko chini ya uongozi wa Wilaya. Yeye alikuwa chanzo cha kheri na baraka, na mfano wa maadili na uchamungu.
Mimi, kwa unyenyekevu, nawasilisha rambirambi zangu kwenu na familia tukufu ya marehemu, seminari (hawza) za kielimu, na wapenzi wote wa marehemu. Na ninamuomba Mwenyezi Mungu ainue daraja ya roho safi ya Marehemu, amuunganishe na Maimamu wake wapendwa huko Akhera. Na pia namuombea Mwenyezi Mungu kwa ajili ya wafiwa wote awajaalie kuwa na Subira njema na ujira mkubwa.
Reza Ramezani
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s)
Your Comment