16 Septemba 2025 - 17:44
Ujumbe wa rambirambi wa Ayatollah Faqihi kwa mnasaba wa kufariki kwa Ayatollah Mousavi Yazdi

Ayatollah Mohsen Faqihi ametuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Mali (Wujuhat) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Ayatollah Mohsen Faqihi, msomi wa ngazi za juu katika Chuo cha Dini cha Qom, alituma ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi, aliyekuwa mkuu wa ofisi ya masuala ya kifedha (wujuhat) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Andiko la ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kufariki kwa mwanazuoni mcha Mungu na mwenye tabia njema, Mheshimiwa Ayatollah Haj Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi (rahimahullah), ambaye alikuwa miongoni mwa hazina kubwa ya kiroho na kielimu ya Hawza Tukufu ya Qom, kumeleta huzuni na majonzi makubwa.
"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea."

Marehemu huyo mtukufu alitumia maisha yake tukufu katika kujifunza na kufundisha elimu ya Ahlul-Bayt (a.s) na kueneza hukumu na mafundisho ya mwangaza ya Uislamu. Kwa miaka mingi alinufaika na masomo ya wanazuoni na wanavyuoni wakubwa kama Ayatollah Boroujerdi, Ayatollah Araki, na Imam Khomeini (qaddasallahu asraarahum).

Kwa uaminifu na uchaji wake mkubwa kwa Mungu, alikuwa mwanazuoni anayeaminika na kuheshimiwa na wanazuoni wote wa Hawza Tukufu, na alihesabiwa kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri.

Maisha yake yaliyojaa uchaji, unyenyekevu na ikhlasi, pamoja na mafundisho yake yenye thamani katika Hawza ya Qom, ni urithi adhimu kwa walimu, wanafunzi na wanavyuoni wa chuo hicho cha dini.

Mimi, kwa dhati ya moyo wangu, nawasilisha rambirambi zangu kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Ayatollah Khamenei), Marjaa wa kidini, Hawza za elimu, familia tukufu ya marehemu, na watoto wake wapendwa.
Namuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampe marehemu huyo msamaha, rehma na radhi Zake, na awape wafiwa subira njema na ujira mkubwa.

Mohsen Faqihi
22 Rabi’ al-Awwal 1447 Hijria

Ikumbukwe kwamba Ayatollah Sayyid Ali Akbar Mousavi Yazdi, aliyekuwa miongoni mwa wanazuoni wa Hawza ya Qom, mwalimu wa fiqhi na usuli, na mkuu wa ofisi ya wujuhat ya Kiongozi Mkuu, alifariki dunia jana, Jumanne 24 Shahrivar 1404 (kulingana na kalenda ya Iran), baada ya miaka mingi ya juhudi za kielimu na kidini.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha