Mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarallah ya Yemen, Mohammed al-Bukhaiti, amesema kuwa miundombinu muhimu ya Saudi Arabia inaweza kulengwa katika majibu yao yajayo, akieleza kuwa maeneo hayo yanachukuliwa kuwa malengo halali kwa mujibu wa msimamo wa harakati hiyo.
Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama amepokelewa katika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA na Mwenyekiti wake Sheikh Profesa Alhad Mussa Salum, ambapo wamejadili umuhimu wa ushirikiano katika kuimarisha amani, maridhiano na mshikamano wa kitaifa.