14 Julai 2026 - 21:42
Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama Apokelewa Katika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama amepokelewa katika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA na Mwenyekiti wake Sheikh Profesa Alhad Mussa Salum, ambapo wamejadili umuhimu wa ushirikiano katika kuimarisha amani, maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama, amepokelewa katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Profesa Alhad Mussa Salum.

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama Apokelewa Katika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA

Mapokezi hayo (kama ilivyodokezwa hapo juu) yalifanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya JMAT-TAIFA, ambapo pande hizo zilipata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu amani, maridhiano, mshikamano wa kitaifa na kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi Jamii na taasisi za kidini katika kuendelea kuhamasisha jamii kudumisha utulivu, maadili na amani nchini.

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama Apokelewa Katika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA katika bayani yake alisisitiza kuwa JMAT inaona na inaendelea kuona umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa dini, taasisi za Serikali na Wananchi katika kujenga jamii yenye umoja, maridhiano na amani endelevu.

Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama Apokelewa Katika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha