Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) –ABNA– Makao ya mwisho ya duniani ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Husseini Khamenei, pamoja na familia yake iliyopata shahada, yamegeuka kuwa kituo cha kumbukumbu, dua na heshima kwa mamilioni ya wapenzi wake.
Tangu kuzikwa kwake, eneo hilo limekuwa mahali ambapo waumini na wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s.) hufika kutoa salamu zao za mwisho, kusoma Surat al-Fatiha na kumuombea rehema, huku wakihuisha kumbukumbu ya maisha yake ya kujitolea kwa Uislamu, umoja wa Umma na kutetea waliodhulumiwa.
Wafuasi wake wanaeleza kuwa eneo hilo litabaki kuwa alama ya heshima kwa kiongozi huyo shahidi, ambapo kila salamu, dua na moyo wenye shauku ya kumkumbuka utapata nafasi ya kuungana na kumbukumbu yake. Pia wanasisitiza kuwa urithi wake wa kielimu, kiroho na kimapambano utaendelea kuhamasisha vizazi vijavyo katika kushikamana na haki, uadilifu na maadili ya Kiislamu.
Your Comment