Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) –ABNA– Swala ya maiti imesaliwa kwa mwili wa Imam Mujahid Shahidi, Ayatollah Mkuu Sayyid Ali Husseini Khamenei, ikiongozwa na Ayatollah Sayyid Muhammad Taqi Al-Hakim ndani ya Haram Tukufu ya Amirul Muuminiin Imam Ali (a.s.) mjini Najaf, Iraq, tarehe 8 Julai 2026.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya wanazuoni wa Kiislamu, wanafunzi wa elimu ya dini, viongozi wa dini na waumini kutoka maeneo mbalimbali, waliokusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo.

Washiriki walimwombea marehemu rehema na daraja ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza njia ya kujitolea, kusimamia haki na kutetea wanyonge ambayo waliieleza kuwa aliisimamia katika maisha yake.

Hafla hiyo ilifanyika katika mazingira ya huzuni na dua, ambapo waombolezaji walionesha mshikamano wao kupitia kaulimbiu "Simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu" pamoja na "Mazishi ya Imam wa Wanyonge", wakitoa heshima na kumuombea maghfira marehemu.

Your Comment