Mwili mtukufu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei, pamoja na miili ya mashahidi wa familia yake, umefikishwa katika Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) mjini Karbala, ambako maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo.

8 Julai 2026 - 11:17

Mwili wa Kiongozi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei Wafikishwa katika Haram ya Imam Hussein (a.s.) Karbala +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mwili mtukufu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei, pamoja na miili ya mashahidi wa familia yake, umefikishwa katika eneo la Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) mjini Karbala, Iraq, kwa ajili ya marasimu ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho.

Maelfu ya wananchi wa Iraq wamejitokeza katika Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) kushiriki katika marasimu hayo ya maombolezo, wakitoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi wa Umma wa Kiislamu na mtetezi wa wanyonge, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei (Allah Amrehemu), ambaye alijitolea maisha yake katika kuitumikia dini ya Uislamu, Waislamu na kutetea haki za waliodhulumiwa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha