6 Julai 2026 - 20:08
Wanafunzi na Walimu wa Al-Mustafa Zanzibar Wafanya Khatmu ya Qur'an kwa ajili ya Roho za Mashahidi

Kikao maalumu cha khatma ya Qur'ani Tukufu kimefanyika katika Ofisi ya Al-Mustafa Zanzibar kwa ushiriki wa walimu na wanafunzi, kwa ajili ya kumuombea rehema Kiongozi Shahidi wa Umma wa Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na Mashahidi wote wa Vita vya Ramadhani.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Walimu na wanafunzi wa Ofisi ya Al-Mustafa Zanzibar wamekusanyika katika kikao maalumu cha khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kumuombea rehema na daraja za juu kiongozi shahidi wa Umma wa Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na Mashahidi wote wa Vita vya Ramadhani.

Wanafunzi na Walimu wa Al-Mustafa Zanzibar Wafanya Khatma ya Qur'ani kwa ajili ya Roho za Mashahidi

Washiriki wa kikao hicho walisoma Qur'ani Tukufu, wakamwomba Mwenyezi Mungu Awajaalie mashahidi hao rehema, msamaha na daraja ya juu Peponi, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano wa Kiislamu, kushikamana na mafundisho ya Qur'ani na kuenzi kujitolea kwa mashahidi katika kulinda dini na haki.

Wanafunzi na Walimu wa Al-Mustafa Zanzibar Wafanya Khatma ya Qur'ani kwa ajili ya Roho za Mashahidi

Kikao hicho kilihitimishwa kwa dua maalumu ya kuwaombea Waislamu amani, umoja na ushindi dhidi ya dhuluma.

Wanafunzi na Walimu wa Al-Mustafa Zanzibar Wafanya Khatma ya Qur'ani kwa ajili ya Roho za Mashahidi

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha