Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Austria amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sasa imekuwa moja ya nguvu kubwa duniani kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za kimataifa.
Alisema kuwa Iran ilionyesha ustahimilivu wa hali ya juu mbele ya kile alichokitaja kuwa uchokozi wa Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, jambo lililoifanya ipate heshima kubwa zaidi katika jumuiya ya kimataifa na kuvunja simulizi ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikitawala kuhusu taifa hilo.
Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo, mafanikio hayo yameifanya Washington kuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa, huku ushawishi wa Iran ukiendelea kuongezeka katika siasa za kimataifa.
Aidha, alieleza kuwa mwelekeo wa Umoja wa Ulaya umebadilika kutoka kaulimbiu ya "tufanye biashara pamoja" kwenda "tujiandae kwa vita", hali ambayo inaashiria mabadiliko makubwa katika sera za kisiasa na kiusalama barani humo.
Your Comment