Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Austria amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejidhihirisha kama nguvu kubwa ya kimataifa baada ya kuonyesha uimara mkubwa dhidi ya kile alichokiita uchokozi wa Marekani, akisisitiza kuwa hali hiyo imeibua hofu mjini Washington na kubadili mwelekeo wa Ulaya kutoka ushirikiano wa kibiashara kwenda kwenye maandalizi ya vita.
Kutokana na ongezeko la idadi ya Waislamu nchini Austria, shirika la habari linalopingana na Uislamu, Rair Foundation, limechapisha video kutoka moja ya mtaa wa Vienna, likidai kwamba ongezeko la idadi ya Waislamu linaelekea kubadilisha Vienna, vizazi viwili vijavyo, kuwa jiji lenye Waislamu wengi.