zamani
-
Taliban: Pakistan imemuua Jenerali Ikramuddin Saree kwa mauaji ya kulengwa Jijini Tehran
Taliban imedai kuwa Pakistan, kupitia shirika lake la ujasusi la ISI, ilihusika na mauaji ya kulengwa ya Jenerali Ikramuddin Saree Jijini Tehran. Kwa mujibu wa vyanzo vya kiusalama, mauaji hayo yalilenga kuvuruga uhusiano kati ya Kabul na Tehran, na tukio hilo bado linaendelea kuibua mjadala na tahadhari za kiusalama.
-
Balozi Matinyi Auvunja Msimamo wa Kibeberu: Tanzania Si Taifa la Huruma, Bali Nguvu Inayoinuka Kiuchumi
Katika ujumbe wake mzito kwa jumuiya ya kimataifa, Balozi Matinyi alisisitiza kuwa Tanzania ya sasa inatafuta wafanyabiashara na wawekezaji, si wafadhili. Taifa linaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), pamoja na mradi wa gesi asilia unaokadiriwa kugharimu dola bilioni 42, miradi inayolenga kuimarisha uchumi wa taifa na nafasi yake katika uchumi wa kikanda na kimataifa.
-
Mwisho mchungu wa ushirikiano wa askari wa Afghanistan na serikali ya Marekani
Wanajeshi wa zamani wa Afghanistan ambao walikuwa wakishirikiana na shirika la ujasusi la Marekani, baada ya miaka mingi ya huduma, sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa wakiwa nchini Marekani.
-
Sharīatmadār katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya “Wakili”:
Sayyid Isa Tabatabaei alipuliza roho ya mapambano ndani ya mwili wa jamii ya Kishia / Maadamu kuna uvamizi, basi mapambano yataendelea kuwa hai
Balozi wa zamani wa kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon na mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: “Ikiwa Imam Musa Sadr alikuwa mwanzilishi wa taasisi za kijamii na kitamaduni za Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepuliza roho ya mapambano ndani ya jamii ya Kishia na kuifanya roho hiyo kuwa sehemu ya utambulisho wao. Kutokana na jitihada zake, ndipo mapambano ya kisasa ya Lebanon yalipozaliwa - mapambano ambayo baadaye yalifikia kilele chake katika kuunga mkono dhana na malengo ya Palestina.”
-
Mfumo wa Mahakama wa Serikali ya Joulani umetoa amri ya kukamatwa pasina kuwepo (arrest in absentia) dhidi ya Rais wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad
Hapo awali, mfumo wa mahakama wa Ufaransa katika Mwezi wa Novemba 2023, uliitoa hukumu ya kukamatwa dhidi ya Bashar Assad kwa ushiriki katika mashambulizi ya kemikali yaliyotolewa na majeshi yake mwaka 2013 katika Ghouta na maeneo mengine karibu na Damascus, yaliyopelekea vifo vya watu wengi.