11 Julai 2026 - 09:54
Chuo cha Al-Mustafa (s) Tanzania Kuaandaa Kongamano la Kielimu Kumuenzi Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei(ra)

Kitengo cha Utafiti wa Kisayansi cha Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s) Tawi la Dar es Salaam - Tanzania kitaandaa Kongamano la Kielimu lenye anuani "Imam Khamenei: Kutoka Jihadi hadi Ushahidi," likiwa na lengo la kuchambua kwa ufupi Maisha ya Kiongozi huyo wa Mapinduzi ya Kiislamu, na hatimaye kukuachia msikilizaji na mfuatiliaji Nafasi ya kupata mazingitio na masomo mbalimbali ya kimaisha kutoka katika kumbukumbu ya Maisha yake Matukufu, katika muktadha ule ule wa Maelekezo ya Qur'an Tukufu aliposema Mwenyezi Mungu: Hakika kuna mazingatio ndani ya visa vyao (Historia Yao) kwa watu wenye Akili"

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kitengo cha Utafiti wa Kisayansi cha Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s) Tawi la Dar es Salaam, Tanzania, kitaandaa kongamano la kielimu lenye anuani: "Imam Khamenei: Kutoka Jihadi hadi Ushahidi (Shahada) – Uchambuzi Mfupi wa Maisha ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu."

Mara hiyo katika Kongamano hilo itawasilishwa na Sheikh Dkt. Swaleh Maulid, ambaye atatoa uchambuzi kuhusu safari ya maisha ya Imam Khamenei, mchango wake katika harakati za Mapinduzi ya Kiislamu, nafasi yake katika uongozi wa Umma wa Kiislamu, pamoja na urithi wake wa kielimu, kiroho na kisiasa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na waandaaji, kongamano hilo litafanyika Jumamosi, tarehe 11 Julai 2026, kuanzia saa 4:00 hadi saa 5:30 asubuhi, katika Msikiti (Muswalla) wa Chuo cha Al-Mustafa (s), Dar es Salaam.

Waandaaji wamewahimiza wanafunzi, walimu, wasomi na wadau wa elimu pamoja na jamii kwa ujumla kushiriki katika kongamano hilo la kielimu ili kujifunza kwa kina kuhusu maisha, fikra na mchango wa Imam Khamenei katika kuimarisha Uislamu na umoja wa Umma wa Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha