Uchambuzi
-
Chuo cha Al-Mustafa (s) Tanzania Kuaandaa Kongamano la Kielimu Kumuenzi Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei(ra)
Kitengo cha Utafiti wa Kisayansi cha Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s) Tawi la Dar es Salaam - Tanzania kitaandaa Kongamano la Kielimu lenye anuani "Imam Khamenei: Kutoka Jihadi hadi Ushahidi," likiwa na lengo la kuchambua kwa ufupi Maisha ya Kiongozi huyo wa Mapinduzi ya Kiislamu, na hatimaye kukuachia msikilizaji na mfuatiliaji Nafasi ya kupata mazingitio na masomo mbalimbali ya kimaisha kutoka katika kumbukumbu ya Maisha yake Matukufu, katika muktadha ule ule wa Maelekezo ya Qur'an Tukufu aliposema Mwenyezi Mungu: Hakika kuna mazingatio ndani ya visa vyao (Historia Yao) kwa watu wenye Akili"
-
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi: Marekani Inaelewa Zaidi Lugha ya Uchumi Kuliko Ahadi za Kisiasa
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mohammad Mokhber, amesema Iran haitakubali makubaliano yasiyotekelezwa kikamilifu na kusisitiza kuwa haki za wananchi wa Iran pamoja na damu za mashahidi haziwezi kusahaulika.
-
Jarida la Foreign Affairs: "Uwezo wa Marekani Hautoshi Tena Kutimiza Malengo Yake ya Kimataifa"
Uchambuzi wa jarida la Foreign Affairs unasema kuwa kuongezeka kwa vitisho katika Mlango wa Hormuz na maendeleo ya teknolojia za kijeshi kumeonyesha pengo kati ya matarajio ya kimataifa ya Marekani na uwezo wake halisi wa kudhibiti usalama wa bahari duniani.
-
Mchezo wa Subira na Mizania; The Guardian yaangazia mtindo wa mazungumzo wa Abbas Araghchi kuelekea mazungumzo ya nyuklia
Uchambuzi wa The Guardian unaeleza kuwa Abbas Araghchi anatumia mkakati wa subira na mizania katika mazungumzo ya nyuklia, huku ukilinganisha diplomasia ya Iran na mchezo wa chess na ile ya Donald Trump na mieleka, na kubainisha kuwa mafanikio yatategemea hatua za pamoja zisizoweza kubadilishwa.
-
Kuanzia Panama 1989 hadi Venezuela 2025; Kurudiwa kwa Sera ya Uingiliaji wa Marekani katika Amerika ya Kusini
Uingiliaji huu, ambao mara nyingi umelaaniwa na jumuiya ya kimataifa, umezaa matokeo ya kudumu kama vile ukosefu wa utulivu, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kudhoofishwa kwa uhuru wa mataifa - hali inayosisitiza tena umuhimu wa kuheshimu sheria za kimataifa na kupinga sera za upande mmoja zinazoathiri amani ya kikanda.
-
Uchambuzi wa ramani ya Israel: Kutoka Ghaza na Ukanda wa Magharibi hadi Syria katika kivuli cha ukimya na Vita Baridi
Baada ya tangazo la mapumziko ya silaha, umakini wa kimataifa kwa Ghaza ulipungua, na kuipa Israel nafasi ya kuchukua hatua bila shinikizo lolote la kweli. Uchambuzi huu unaisha kwa onyo kwamba kimya cha kimataifa kinachoendelea hakiondoi uwezekano wa mlipuko wa hali hiyo, bali kinariongeza.
-
Uchambuzi na Tathmini ya Thawabu za Ajabu na za Kipekee kwa Matendo Rahisi
Kuwepo kwa thawabu kubwa kwa baadhi ya matendo rahisi ni jambo lisilopingika, kwa sababu mizani ya Mwenyezi Mungu katika kutoa malipo haifanani na mizani ya kidunia.
-
Iran Yazalisha Dawa ya Kuzuia Leukemia;
Dawa ya Kuzuia Leukemia ya Iran Yapunguza Gharama ya Matibabu kwa 95%
Maendeleo haya ni kielelezo cha hatua muhimu kwa Uhuru wa bioteknolojia na huduma za afya za Iran, yakionyesha mabadiliko yanayoendelea ya uchumi wa maarifa (iqtisad-e danesh-bonyan).
-
Sisi na wamagharibi kwa Mtazamo wa Imam Khamenei – Mkutano Uliofanyika Nchini Kenya +Picha
Pourmarjan: “Ayatollah Khamenei, kama mwanafiqhi na mwanafikra mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu, na ambaye ametumia zaidi ya miaka sitini katika nyanja za kielimu, kidini, kitamaduni, na kisiasa, ametoa mitazamo sahihi na ya kimkakati kuhusu Magharibi. Uelewa wa fikra hizi ni muhimu sana kwa kizazi cha leo cha vijana na wasomi.”
-
Kikundi cha “Abu Shabab” Kusini mwa Ukanda wa Gaza kiko katika hali ya kusambaratika
Kikundi cha wanamgambo kinachoitwa “Abu Shabab” kiko karibu kabisa kuvunjika baada ya kupoteza msaada wa anga kutoka kwa Israel na kushambuliwa kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa Harakati ya Hamas.