Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa mujibu wa Shirika la habari la Fars, utawala wa Kizayuni wa Israel hutumia mfumo wa Akili Bandia unaoitwa “Gospel” kwa ajili ya kutambua majengo yanayolengwa kushambuliwa katika mashambulizi ya anga. Tofauti na mfumo mwingine wa AI uitwao “Lavender” unaotumika kwa kuorodhesha watu kwa ajili ya kuuawa, “Gospel” hulenga majengo na miundombinu kama vile nyumba, ofisi, na vituo vya mawasiliano. Mfumo huu hukusanya na kuchanganua taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kama vile:
1- Ufuatiliaji wa mawasiliano yanayopatikana katika jengo husika.
2- Picha za satelaiti.
3- Harakati na nafasi ya watu wanaoshukiwa kuingia au kutoka ndani ya majengo hayo.
Baada ya uchambuzi wa mfumo huo wa Akili Bandia, jengo hupewa "kiwango cha hatari (uwiano wa hatari)" (risk coefficient). Mfumo huo haufanyi maamuzi kwa uhakika, bali hufanya kwa msingi wa makadirio. Kwa mfano: Hata kama kuna asilimia 50 tu ya uwezekano kuwa jengo linahifadhi silaha, linaweza kulengwa na kushambuliwa.
Hali hii imekosolewa vikali na wataalamu wa Kimagharibi kwa sababu inaweza kusababisha makosa makubwa na kuua raia wasio na hatia kwa idadi kubwa.
Mfumo huu ulitumika kwa kiwango kikubwa kwenye mashambulizi ya mwaka 2023 dhidi ya Gaza ambapo majengo kadhaa yalishambuliwa kwa wakati mmoja kwa kisingizio cha uwepo wa wapiganaji wa Hamas ndani yake.
Kwa kuzingatia mashambulizi ya karibuni ya anga dhidi ya maeneo ya makazi nchini Iran, kuna uwezekano mkubwa kuwa mfumo wa “Gospel” ulitumika, ingawa mamlaka rasmi bado hazijathibitisha hilo.
Israel inaendesha “viwanda vya zana za mauaji” kupitia vitengo kama vile Unit 8200 ya jeshi lake, ambayo imeunda mifumo mingine ya AI kama:
1- Depth of Wisdom: Kuchambua mifereji ya ardhini (tunnel modeling)
2- Alchemist: Kutambua vitisho vya ardhini.
3- Where’s Daddy: Kufuatilia simu za mkononi za watu wanaoshukiwa.
Suluhisho linalopendekezwa ni kuimarisha usalama wa taarifa na mazingira ya kidijitali ili kuepuka kuua watu hovyo wasiokuwa na hatia, na hiyo ni jinai ya kivita na iko kinyume na haki za binadamu, bali ni kinyume na sheria za umoja wa mataifa.
Your Comment