Kamanda wa Vikosi vya Ardhi vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Mohammad Karami, amesema vikosi vyao vinaendelea kuwa katika kiwango cha juu cha utayari wa kiintelijensia na kiutendaji ili kukabiliana na tishio lolote kutoka kwa maadui wa nje au makundi ya kigaidi.
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Hussein Mohabbi, amesema Marekani itajutia endapo itajaribu kurudia kile alichokiita majaribio yake yaliyoshindwa dhidi ya Iran.
Mark Kenny, Profesa wa Masomo ya Australia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Australia (Australian National University), ameonyesha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa hatari ya chuki dhidi ya Uislamu baada ya shambulio la Sydney na kutoa onyo kuhusu suala hilo.