Mkuu
-
Telegraph: Tuhuma za Israel dhidi ya Hezbollah na Iran katika mauaji ya Bondi hazina ushahidi wa kuthibitishwa
Gazeti la Telegraph limeripoti kuwa Israel imehusisha mauaji ya Bondi na Hezbollah pamoja na Iran bila kuwasilisha ushahidi wa kuaminika, huku maafisa wa Australia wakiwa hawajathibitisha ushiriki wowote wa nje, na uchunguzi ukiendelea.
-
Mufti Mkuu wa Australia alilaani shambulio la silaha huko Sydney
Mufti Mkuu wa Australia na New Zealand amelilaani vikali shambulio la silaha lililotokea katika Ufukwe wa Bondi, Sydney, na kulitaja kuwa ni kitendo cha kigaidi.
-
Tamko la Mkurugenzi Mkuu wa Hawza za Kiislamu Kufuatia Mauaji ya Kinyama Dhidi ya Watu Wanyonge wa Sudan
Jumuiya za Kimataifa na Mashirika ya Haki za Binadamu Waitikie Kilio cha Watu Wanaodhulumiwa Sudan
-
Jeshi la Israel Ladai Kumuua Kigaidi Kamanda Mwandamizi wa Hezbollah katika Mji wa Beirut
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Aljazeera, jeshi la Israel limedai kuwa limemuua mmoja wa makamanda wakuu wa Hezbollah katika mji wa Beirut.
-
Mkutano wa Kundi la Viongozi wa Kidini wa Kishia na Askofu Mkuu Mpya wa Washington
Kikundi cha viongozi wa kidini wa Kishia nchini Marekani pamoja na Askofu Mkuu wa Washington wamekutana katika kikao cha kirafiki ili kuimarisha ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo na kupanua njia za mazungumzo ya baina ya dini mbalimbali.
-
Ujumbe wa rambirambi wa Ayatollah Ramezani kwa Mkuu wa Haram ya Kudumu ya Razavi
Ayatollah Ramezani katika ujumbe wake aliweka rambirambi kwa kifo cha dada wa Ayatollah Marvi.
-
Sharīatmadār katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya “Wakili”:
Sayyid Isa Tabatabaei alipuliza roho ya mapambano ndani ya mwili wa jamii ya Kishia / Maadamu kuna uvamizi, basi mapambano yataendelea kuwa hai
Balozi wa zamani wa kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon na mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: “Ikiwa Imam Musa Sadr alikuwa mwanzilishi wa taasisi za kijamii na kitamaduni za Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepuliza roho ya mapambano ndani ya jamii ya Kishia na kuifanya roho hiyo kuwa sehemu ya utambulisho wao. Kutokana na jitihada zake, ndipo mapambano ya kisasa ya Lebanon yalipozaliwa - mapambano ambayo baadaye yalifikia kilele chake katika kuunga mkono dhana na malengo ya Palestina.”
-
Qalibaf: Pakistan ni rafiki wa kweli katika nyakati zote
Spika wa Bunge la Iran ameandika kwenye ukurasa wake binafsi katika mitandao ya kijamii kuwa:“Kwa mwaliko maalumu wa Mheshimiwa Spika wa Bunge la Kitaifa la Pakistan, nimeelekea nchini humo. Kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya mataifa haya mawili ndugu - hususan katika nyanja za ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama - kutakuwa ndiyo mhimili mkuu wa ziara hii.”
-
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC): Tukivamiwa, tutawasha moto wa Jahannam dhidi ya wavamizi
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Mohammad Pakpour, katika mazungumzo na Qasim al-A’araji, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq, amesema kuwa: “Katika vita vya siku 12, tulishambulia kwa nguvu na usahihi mkubwa na tuliharibu malengo yote yaliyolengwa.”
-
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu:“Wazayuni hawakutarajia nguvu ya makombora ya Iran / Marekani haina haki kujihusisha na teknolojia ya Iran"
Ayatollah Sayyid Ali Khamenei amebainisha kwamba: Marekani haina haki kujihusisha na suala la teknolojia ya nyuklia ya Iran - na akahoji kuhusiana na Trump akisema: Wewe ni nani hasa?”.
-
Mkuu wa Majeshi: Vikosi vya Ulinzi vya Iran Vitatoa Jibu Kali Zaidi ya Mawazo ya Wavamizi
“Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa mwongozo wa Kiongozi Muadhamu Ayatollah Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde), vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko tayari kugeuza tishio lolote kuwa fursa ya kustawisha nguvu za taifa na kuinua hadhi ya Iran katika mizani ya kimkakati ya kikanda na kimataifa. Jibu letu kwa maadui litakuwa la wakati, kali, la kuumiza na zaidi ya walivyowahi kufikiria.”
-
Kuimarishwa kwa hatua za kiusalama katika mji mkuu wa Iraq kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu
Kamanda wa operesheni za Baghdad ametangaza kuanza kwa mpango mpya wa kukabiliana na wizi wa magari na mauaji katika mji mkuu wa Iraq.
-
Ujumbe wa rambirambi wa Ayatollah Faqihi kwa mnasaba wa kufariki kwa Ayatollah Mousavi Yazdi
Ayatollah Mohsen Faqihi ametuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Mali (Wujuhat) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
-
Amir Pourdastan: Moyo wa taifa la Iran unapaswa kujitolea kwa vikosi vya jeshi
Mkuu wa Kituo cha Tafiti za Kimkakati cha Jeshi alisema: Wananchi wa Iran wawe na moyo thabiti na wawe na utulivu, na wafahamu kuwa watoto wao na ndugu zao walioko jeshini wana ujuzi na maandalizi ya kutosha.
-
Spika Mike Johnson Asisitiza Kuzuia Vurugu za Kisiasa Kufuatia Kifo cha Charlie Kirk
Shambulio dhidi ya Qatar lisingeweza kutokea bila kupata idhini kutoka Washington.