10 Desemba 2025 - 18:27
Tamko la Mkurugenzi Mkuu wa Hawza za Kiislamu Kufuatia Mauaji ya Kinyama Dhidi ya Watu Wanyonge wa Sudan

Jumuiya za Kimataifa na Mashirika ya Haki za Binadamu Waitikie Kilio cha Watu Wanaodhulumiwa Sudan

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Ayatullah A'rafi amesema: “Katika wakati ambao Umma wa Kiislamu unahitaji zaidi umoja, mshikamano na kurejea kwenye misingi ya utu na maadili ya Kiungu, taarifa za kutisha kuhusu mauaji ya kinyama na ya kikatili dhidi ya watu wanyonge wa Sudan zimeumiza na kuchoma mioyo ya kila mwanadamu huru na mwenye dhamiri.”

◽️Amebainisha kuwa tukio hili la umwagaji damu, ambalo limefanyika kwa ushiriki na uungaji mkono wa moja kwa moja wa uzayuni wa kimataifa na ubeberu wa dunia, sambamba na ushirikiano wa kusikitisha wa baadhi ya tawala za Kiarabu katika eneo la Ghuba, ni mfano wa wazi wa miradi ovu ya maadui wa Umma wa Kiislamu inayolenga kueneza mifarakano, kupora rasilimali za mataifa na kudhoofisha harakati za mwamko wa Kiislamu.

◽️Hawza za kielimu na wanazuoni wa Kiislamu, sambamba na kulaani vikali jinai hii ya kutisha, zinayataka mataifa ya Kiislamu na wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu kutoendelea kukaa kimya mbele ya maafa kama haya. Wanahimizwa kufichua mikono michafu ya madola ya kibeberu na vibaraka wao katika eneo, na kusimama kidete kulinda misingi ya uhuru, heshima na uadilifu katika nchi za Kiislamu.

◽️Kadhalika, inatarajiwa kwamba jumuiya za kimataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), na taasisi za haki za binadamu zitachukua msimamo wa wazi na madhubuti dhidi ya janga hili la kibinadamu, badala ya kimya kizito na kushindwa kuchukua hatua ambako kunatia aibu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha