Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA-baada ya kifo cha mke wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Khamenei, alituma ujumbe wa rambirambi na kutoa pole zake kwa kiongozi huyu wa kidini.
Andiko la ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Mheshimiwa Ayatollah Sayyid Ali Sistani (Baraka zake Zidumu).
"Kufuatia kifo cha mke wako Mtukufu ninakufikishia rambirambi zangu za dhati. Na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Amrehemu na Amsamehe Marehemu huyo".
Your Comment